Mtoto
wa miezi miwili (jina limehifadhiwa) mkazi wa Manispaa ya Shinyanga
amedaiwa kunyeshwa sumu na baba yake mzazi kwa madai ya kutaka kuficha
kizazi hicho ili mkewe asijue amezaa nje ya ndoa.
Akielezea
makasa huo jana, mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Shija (22) alisema
lilitokea Machi 24, mwaka huu majira ya saa tatu usiku.
Maria
alisema siku hiyo baba wa mtoto huyo, Edson Damian (37) alikwenda
nyumbani kwao anapoishi yeye na mama yake kwa ajili ya kumsalimia mtoto
huyo, na ndipo akamywesha sumu ya panya kwa lengo la kumuua wakiwa
wamekaa nje.
Mzazi
huyo alisema kabla ya mzazi mwenzake kufanya kitendo hicho, alikuwa
akimtuma maji ya kunywa ndani mara kwa mara kitu ambacho si kawaida
yake.
Alisema
aliporudisha kikombe ndani mara ya mwishho ndipo akasikia harufu ya
sumu ya panya, na aliporudi haraka kwa mtoto akamkuta ameanza kutoa
mapovu na mwanaume huyo kukimbia.
“Baada
ya kuona mtoto kapewa sumu nikakimbia kwa jirani ambaye ana zizi la
ng’ombe, ndipo nikachukua maziwa nikamnywesha na baadae nikachukua
bodaboda hadi kituo cha Polisi kupewa RB na kisha kwenda hospitali ya
Rufani ya mkoa wa Shinyanga kupatiwa matibabu," alisema Maria.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi Simon Haule alithibisha
kutokea kwa kisa hicho na kwamba mtuhumiwa huyo yupo mbaroni.
Alisema upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.
Akielezea
historia ya mapenzi yao, Maria alisema Damian wakati anamtaka kimapenzi
alimwambia hana mke, lakini baada ya mtoto kuzaliwa akasema ana mke,
hamtaki kwani atavunja ndoa yake.
Mtu wa karibu na familia ya Maria, Jumanne Kagusa alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi.
No comments:
Post a Comment