Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama amewageukia viongozi
wa dini mbalimbali na kuwasii waendelea kuliombea taifa ili iweze
kudumishwa amana na utulivu huku akiwapongeza uongozi wa Kanisa la
Baptist nchini kwa kuendelea kufanya hivyo.
Waziri
Mhagama anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu nchini ametoa pongezi hizo alipokutana na uongozi wa
Kanisa hilo Bungeni Dodoma ili kujadili na kuipongeza serikali kwa
juhudi inazozifanya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu
kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.
"Niwapongeza
sana uongozi wote wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kutuombea
na kuikumbuka nchi yetu kwani bila uwepo wa amani na utulivu maendeleo
hayawezi kuwepo", amesema Waziri Mhagama.
Aidha,
Waziri Mhagama amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali
katika kuhakikisha inaboresha na kuleta maendeleo ya nchi yake bado kuna
umuhimu wa kuendelea kuwa na ushirika mzuri na viongozi wa dini na
kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt.John Magufuli katika kufikia azma
yake ya "Tanzania ya Viwanda".
"Kipekee
niwashukuru kwa kuona umuhimu wa kutuweka mikononi mwa Mungu uongozi
wote wa nchi, kuanzia kwa Mhe. Rais wetu, Baraza la Mawaziri na viongozi
wote kwa ujumla wao, ili kuhakikisha tunakuwa na hekima na weredi wa
utekelezaji wa majukumu yetu kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo",
amesisitiza Waziri Mhagama.
Askofu
wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase akifanya maombi kwa kifupi
walipomtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama kuzungumza masuala
yao na kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada za kukuza
uchumi na maendeleo kwa ujumla.
Pamoja
na hilo aliuomba uongozi huo kuendelea kuchangia katika huduma za
kijamii hususani kupitia mchango wanautoa kwa jamii wa kuwa na shule,
vyuo na zahanati zinazohudumia wananchi wanaochangia katika uzalishaji
na maendeleo ya nchi yao.
kwa
upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase
ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa hatua kubwa iliyoifanya katika
kuleta mabadiliko ya kimaendeleo tangu ilipoingia madarakani na kuahidi
kuendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuona nchi inaendelea
na kuondokana na baadhi ya changamoto zilizopo.
No comments:
Post a Comment