Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri
wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema katika Ripoti ya Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Halmashauri zilizopata Hati Safi
zimeongezeka kutoka Halmashauri 81 kwa mwaka 2015/16 mpaka kufikia
Halmashauri 166 (90%) kwa mwaka 2016/17.
Jafo
ameyasema hayo wakati kwa Kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika
katika ukumbi Bunge kuhusu utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo ya CAG
kwa hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka Ulioishia Juni
30, 2017.
Alisema
“napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wenyeviti na Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa maelekezo yao mazuri
yaliyosaidia sana utendaji kazi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na
MSM; Michango yao, ushauri na maelekezo yamewezesha kuongeza Idadi ya
Hati Safi.
Akizungumzia
kuhusu hoja zilizobainishwa katika ropoti ya CAG Mhe. Jafo alisema
tumefanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa katika ripoti zilizopita
ambapo watumishi 434 wamechukuliwa hatua baada ya kubainika kusababishia
halmashauri zao hasara/hoja zisizo za lazima kutokana na kutotekeleza
ipasavyo wajibu wao ama kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu.
“Kati
ya hao 9 wamefukuzwa kazi, Watumishi 210 wamepewa barua za onyo huku
Watumishi 15 wakifikishwa kwenye vyombo vya dola. Watumishi 28
wamesimamishwa kazi, 13 wametakiwa kufidia hasara kutoka kwenye
mishahara yao wengine 4 wameshushwa vyeo na wengine 10 wamebadilishiwa
majukumu” alisema Jafo.
Aliongeza
kuhusu MSM kupokea Fedha pungufu ya Bajeti Iliyoidhinishwa ni kwa
sababu Serikali hutegemea makusanyo ya mapato kutoka vyanzo mbalimbali.
Hivyo, kiasi kinachotumwa kwenye MSM hutegemea mwenendo wa mapato
yaliyopatikana lakini pia fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa na
Serikali kwa mwaka wa fedha uliotaguliwa 2016/17 zimeongezeka
ikilinganishwa na mwaka wa 2015/16.
Kwa
mwaka 2016/17 fedha za miradi ya maendeleo zilizopokelewa na MSM ni
Tsh. 705,927,921,596.20 sawa na 57% ya bajeti iliyoidhinishwa ya Tsh.
1,242,616,839,000 akati mwaka 2015/16, fedha zilizopokelewa zilikuwa ni
Tsh. 390,525,992,297 sawa 39% ya bajeti ya Tsh. 1,010,650,744,099.
Kuhusu
changamoto katika Usimamizi wa Mapato katika Mhe. Jafo alieleza Wizara
imeendelea kuziba mianya ya uvujaji wa mapato kwa kuhakikisha kuwa
Halmashauri zinahamia katika matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa
ukusanyaji wa mapato ujulikanao kama Local Government Revenue Collection
and Information System (LGRCIS) ambapo takwimu zote za mapato
zinatunzwa katika mfumo huo ambao pia umeunganishwa na mashine za
kukusanyia mapato (Point of Sales) zinazotumiwa na Mawakala/Wakusanya
mapato, na hivyo kuiwezesha Halmashauri kufahamu mapato yaliyokusanywa
na Wakala/Wakusanya mapato hao.
Vile
vile, mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya benki, na hivyo kuwezesha
Halmashauri kufahamu kiasi ambacho Wakala/Mkusanya mapato amekiingiza
kwenye akaunti ya benki ya Halmashauri ikilinganishwa na kiasi
alichokusanya. Mpaka sasa, Halmashauri zote 185 tayari zimewekewa mfumo
huu wa LGRCIS.
Wakati
huo huo alieleza Kuhusu Vitabu 379 vya Kukusanyia Mapato ambavyo
havikuwasilishwa kwa Wakaguzi amesema Licha ya kuwa idadi ya
Halmashauri na idadi ya vitabu vya kukusanyia mapato ambavyo
havikuwasilishwa kwa Wakaguzi imepungua kutoka 871 katika Halmashauri
57 kwa mwaka 2015/16 mpaka vitabu 379 katika Halmashauri 21 kwa Mwaka
2016/17, OR – TAMISEMI imeendelea kusimamia maelekezo ya Serikali ya
Halmashauri zote ziachane na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia
stakabadhi/vitabu vya kuandikwa kwa mkono, na badala yake mapato
yakusanywe kwa kutumia mashine za kielektroniki.
Waziri
Jafo alimalizia kwa kutolea ufafanuzi wa Soko la Mwanjelwa –Mbeya na
kusema kuwa OR-TAMISEMI imeanza kuchukua hatua kuhusiana na dosari
mbalimbali zilizojitokeza katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa na kwa
kuanza tulimuomba CAG kufanya ukaguzi maalum na taarifa iliashiria
makosa ya kijinai na tayari Serikali imelifikisha suala hili kwenye
vyombo vya Dola, ambapo pia Wahusika Wakuu wa mikataba husika na
usimamizi wa utekelezaji wake, nao pia wameshafikishwa kwenye vyombo vya
Dola kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi. Serikali itaendelea
kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na CAG ili kuokoa hasara
itokanayo na ujenzi wa soko hilo.
No comments:
Post a Comment