Balozi
wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, ameonya kuwa
shambulio lolote la anga litakalofanywa na Marekani nchini Syria
litasabaisha kulipuka kwa vita baina ya Moscow na Washington na kuongeza
kuwa Urusi haiwezi kuepuka uwezekano wowote wa kutokea vita baina ya
mataifa hayo.
Nebenzia
ameituhumu Marekani na washirika wake kwa kuiweka amani ya mataifa
katika hali hatari zaidi kwa kile alichokiita sera za ukatili na kusema
kuwa hali ilivyo kwasasa ni hatari kupita kiasi.
Aidha,
Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na
viongozi wa mataifa ya Ufaransa na Uingereza kujadili juu ya kutoa kauli
ya pamoja kwa kile wanachoamini kuwa matumizi ya sialaha za kemikali
yaliyofanywa na Syria kwenye maeneo ya kitalii yanayoshikiliwa na waasi.
Hata
hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imesema baraza la mawaziri
limekubaliana kwamba matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria
haipaswi kwenda kinyume lakini hakutoa maelezo ya hatua yoyote inayoweza
kuchukuliwa.
Baada
ya mkutano wa dharula uliochukua saa mbili mjini London, taarifa
isiyorasmi inasema kwamba Theresa May ataendelea kushirikiana kikazi na
nchi za Marekani na Ufaransa ili kuratibu mwitikio wa kimataifa.
Wabunge
kutoka Chama cha upinzani cha Labour pamoja na Chama cha Usimamizi wa
kihafidhina wametaka kura ya turufu ipigwe bungeni kabla ya majeshi ya
Uingereza kuchukua dhamana.
No comments:
Post a Comment