Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema, si watu wote
wanaopoteza maisha katika vituo vya polisi wanakuwa wameteswa.
Waziri
Lugola pia amehoji, kwani nini mtu akipoteza maisha akiwa kituo cha
polisi wananchi wanavamia kituo lakini hawachomi nyumba na kitanda
mwananchi anapoaga dunia wakati anafanya mapenzi.
Ameyasema
hayo bungeni wakati anajibu maswali ya nyongeza ya wabunge kwenye
kikao cha nane cha Mkutano wa 12 wa Bunge unaoendelea jijini Dodoma.
Lugola
amesema, mwananchi anaweza kupoteza maisha wakati wowote na mahalali
popote na ndiyo maana kwenye Biblia imeandikwa kifo ni mtego, humnasa
mtu wakati wowote na mahali popote.
"Kwa
hiyo mwananchi anaweza akafa akiwa polisi, anaweza akafa akiwa anafanya
mapenzi, anaweza akafa akiwa kwenye gari anasafiri, anaweza akafia hata
humu ndani ya Bunge humu. Kwa hiyo isije ikachukuliwa kwamba anayekufia
kwenye kituo cha polisi ni kwamba ameteswa" amesema.
Hata hivyo Waziri Lugola amekiri kuwepo kwa matukio ya wananchi kufia mikononi mwa Polisi.
"Na
pale ambapo matukio hayo yanajitokeza tumekuwa tukifanya uchunguzi. Na
pale inapobainika kwamba Polisi wamehusika tumekuwa tukichukua hatua. Na
ndiyo maana Mheshimiwa Spika tunazuia wananchi wasichukue sheria
mikononi za kuanza kuvamia vituo kwa sababu mtu amefia mikononi mwa
polisi...
"Na
ndiyo maana nimekuwa nikihoji, huyu anayekufa akifanya mapenzi mbona
hawaendi kuchoma kitanda na nyumba kwamba amefia mikoni mwa
kitanda"amesema Lugola.
Wakati
anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga, Waziri
Lugola amesema, Jeshi la Polisi halina nia ya kuwatesa wananchi
wanapokamatwa na kuwekwa mahabusu.
Mbunge huyo alitaka kufahamu kauli ya Waziri Lugola kuhusu mahabusu kukosa chakula.
"Mahabusu
wote wanapata chakula na wapo watu ambao wanapewa tenda hizi za kuleta
vyakula kwa mahabusu"amesema na kuongeza kuwa, kuna wananchi
wanaoruhusiwa kupeleka vyakula kwa mahabusu.
No comments:
Post a Comment