Makamu
wa Rais Samia Suluhu atakuwa mgeni rasmi katika uzunduzi wa tamasha la
urithi litakalofanyika kati ya Septemba 15 hadi 22 mwaka huu jijini
hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Septemba 13 2018, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk
Binilith Mahenge amesema kuwa Samia atamwakilisha Rais John Magufuli
ambaye ndiye awali alikuwa awe mgeni rasmi.
Amesema
maonyesho lengo la tamasha hilo ni kupanua wigo wa vivutio vya utalii
nchini hususani kwa kuendeleza mazao ya utalii, utamaduni na malikale.
“Kauli
mbiu ya maonyesho haya ni ‘Urithi wetu Fahari yetu’ na yatahusisha
wadau kuonyesha mambo ya burudani, maigizo, utalii na tamaduni, malikale
na kazi mbalimbali za mikoa,”amesema.
Amesema
kutakuwa na maandamano yenye shamrashamra za ngoma, machifu, watalii,
washahiri, maigizo, wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi akiwemo
Mrisho Mpoto na Wanne Star.
No comments:
Post a Comment