Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amesema Serikali inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuwaletea
wananchi maendeleo endelevu.
Makamu
wa Rais ameyasema haya jana wakati wa sherehe za kusimikwa wakfu wa
Askofu Mkuu Msaidizi pamoja na Maaskofu wanne wa majimbo wa Kanisa la
Pentekoste Motomoto, Mwanga mkoani Kigoma.
“Serikali
imeweka mazingira rafiki kwa madhehebu ya dini nchini kuweza kutoa
huduma za kijamii hususan elimu na afya” alisema Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais amesisitiza umuhimu wa kanisa kujiepusha na migogoro ya
kiutawala ndani ya Kanisa na pia liepuke kuchanganya dini na siasa
“Kazi
kubwa ya Kanisa iwe kuhubiri Amani kwa waumini wake na wananchi kwa
jumla” alisema Makamu wa Rais huku akinukuu neno la Mungu katika
Waebrania 12:14, ambalo linasema “tafuteni kwa bidii kuwa na Amani na
watu wote”.
Aidha,
Eneo jingine ambalo Serikali inalitegemea Kanisa ni katika kujenga
maadaili mema ya jamii, hivyo Makamu wa Rais alilitaka Kanisa kusaidiana
na Serikali katika kupiga vita tamaduni mbaya za nje ili kujenga Taifa
lenye maadili ya Kitanzania, pia Serikali inalitegemea Kanisa katika
kupiga vita rushwa na ufisadi ambavyo ni adui wa maendeleo ya nchi.
Kwa
upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Baba Askofu Ezra Enock Mtamya
ameupongeza Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi zake za
kuijenga Tanzania yenye maendeleo ambapo pia alisema kama Kanisa
wamekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya jamii na utunzaji wa
mazingira ambapo wameiomba Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais
kuwapa wataalam wa mazingira pamoja na ufugaji nyuki.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amewata
Wanaume wawe mstari wa mbele katika kupima afya zao na kuzingatia lishe
bora kwa watoto.
Maaskofu
waliosimikwa jana ni Askofu Mkuu Msaidizi Bwami J. Mathias, Askofu
Shemu A. Mwenda (Jimbo la Kati), Askofu Simon S. Bikatago wa Jimbo la
Magharibi, Askofu Jackson Maneno wa Jimbo la Tanganyika na Askofu
Eliasaph Mathayo wa Jimbo la Mashariki.
No comments:
Post a Comment