Serikali
imewataka wananchi wanaoishi kuzunguka Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi
waliokuwa wamefungua kesi na baadaye kushindwa waendelee kuheshimu
mipaka ya Msitu huo huku Chama cha Mapinduzi kikiangangalia namna bora
ya kuwasaidia.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Wananchi hao waliokuwa na mgogoro wa Ardhi ndani ya Msitu huo kufungua kesi mwaka 2017, kwenye Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na maamuzi ya shauri la madai hayo yaliipa serikali ushindi, baada ya wananchi hao kushindwa kuonyesha ushahidi wa umiliki wa ardhi ikiwa ni ushahidi wa manunuzi na urithi wa ardhi hiyo katika Msitu wa Hifadhi ya Kazimzumbwi,
Akizungumza
kwenye mkutano na wananchi hao katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala
mkoani Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe.
Wiliam Lukuvi amewaambia wananchi hao kuwa hawana haki kwenye ardhi
hiyo kwa mujibu wa hukumu iliyotoka,
Aliongeza kuwa mipaka ya msitu huo ipo sahihi na si vinginevyo hali iliyopelekea wananchi hao kushindwa kukata rufaa.
Hata
hivyo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
amejipa siku 30 kuangalia namna ya kuwasaidia wakazi hao walioshindwa
kesi.
Ameongeza
kuwa tayari ameshaunda kamati iliyopewa muda wa miezi miwili na tayari
imeshamaliza mwezi mmoja na hivyo itatoa majibu ndani ya siku 30 lengo
likiwa ni kuwasaidia wananchi hao ambao kisheria walishindwa kesi.
"Mgogoro huu ulishafika mahakamani na uamuzi ukatolewa kuwa mmevamia hilo lipo wazi na sisi hatupingani na uamuzi wa mahakama.
"Ila
kwa kuwa nyie ni wananchi wetu, CCM imeamua kununua kesi, sio kwa maana
ya kupinga mahakama Bali ni kwa kuangalia tunawasaidia vipi," alisema
Mhe. Lukuvi
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga
amesema wizara yake haina tatizo na wakazi hao zaidi ya kuhakikisha
msitu huo uko salama.
Amesema katika kipindi ambacho msitu huo ulivamiwa athari kubwa zilijitokeza.
"Msitu
huu tunaweza kusema ndio mapafu ya Dar, sasa ukivamiwa kwa kuwekwa
Makazi au shughuli za kibinadamu mambo yanakuwa mabaya,”
Tunategemea
tupate hewa nzuri kutoka huku lakini wao walivamia na kutengeneza hewa
chafu. Sisi tunachosimamia ni kuhakikisha msitu unatunzwa na kubaki kuwa
msitu,"amesema.
Baadhi
ya wawakilishi wa kundi hilo la wananchi waliokuwa wamevamia msitu
huo wameeleza kuwa wanachotaka ni kuonyeshwa mipaka ya kitaalam ya
unapoanzia msitu huo.
"Hatupingani
na mahakama wala wizara sisi tunataka wataalam wa wizara ya ardhi waje
wafanye vipimo na kutuonyesha kitaalam ilipo mipaka," amesema Jackson
Rwehumbiza.
Akizungumza
kuhusu msitu huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania,
Prof. Dos Santos Silayo alisema, Mwaka 1954 serikali ilianzisha Msitu wa
Hifadhi wa Kazimzumbwi wenye ukubwa wa hekta 4,860, kwa Tangazo la
Serikali Na. 306 la mwaka 1954 na ramani Jb 196 ya mwaka 1954 kwa
kutambua umuhimu wake.
Profesa
Silayo anasema licha ya umuhimu wake Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi
umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na wananchi wanaoishi kuzunguka msitu
huo na serikali ilifanya zoezi la kuwaondoa mwaka 1998,2003,3007,2011 na
2014.
No comments:
Post a Comment