Mkuu
wa kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya klabu ya Simba, Haji
Manara ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini TFF kutumia neno hujuma katika kumpatia adhabu ya kumfungia
mwaka mmoja kutojihusisha na mpira meneja wa timu hiyo, Richard Robert.
Kupitia mahojiano na EFM radio, Manara amesema kuwa lugha ya hujuma iliyotumiwa na TFF siyo nzuri na wanapaswa kuangalia maneno ya kutumia.
”Tunangojea kupokea barua alafu tutalitolea tamko kwa sababu Simba hatuwezi kulikalia kimya hili jambo tutasema ama kukata rufaa ama tutasema lakini kwanza tunasubiri barua,” amesema Haji Manara
Manara ameongeza ”Unajua neno hujuma sijui maana yake, hujuma ni jambo kubwa sana, hujuma ni dhambi kuu sijui, hujuma adhabu yake ni kifo, jeshini kule ukiujumu adhabu yake ni kupigwa risasi sasa hii kwa kutumia neno hujuma peke yake hiyo imetustua watu wote Simba nadhani TFF wataangalia namna sahihi ya kutumia lugha.”
”Lugha za hujuma hazikutufurahisha sana lakini yote kwa yote wacha leo nione barua ikija tutazungumza.”

No comments:
Post a Comment