“Kumekuwa
na raia wengi kutoka Msumbiji katika Jimbo la Mchinga hasa vijiji vya
Kilangala B, Butamba na Mvuleni Kilombwani, wamekuwa wakishiriki
uchaguzi katika nchi zote mbili, je, raia hao ni Watanzania au wa
Msumbiji, na je, Serikali imepitisha utaratibu wa raia pacha na kuwapa
watu maalumu,” amehoji Bobali.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, amesema sheria
hazijaruhusu uraia wa nchi pacha wala hakuna watu maalumu waliopewa
uraia wa aina hiyo.
“Ibara
ya 5 (2) (a) ya katiba hairuhusu mtu mwenye uraia wa nchi nyingine
kushiriki shughuli za uchaguzi ikiwamo kupiga kura, hata hivyo, ili mtu
aweze kupiga kura lazima awe ameandikishwa kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura lililoanzishwa chini ya Ibara ya 5 (3) (a) ya Katiba,”
amesema Mavunde.
No comments:
Post a Comment