Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameagiza
kufukuzwa kazi afisa ardhi wa wilaya ya Monduli bwana Kitundu Mkumbo kwa
kukiuka sheria na taratibu za utoaji wa hati miliki za kimila.
Waziri
Lukuvi ametoa agizo hilo mbele ya wakazi wa kijiji cha Engarooji
wilayani Monduli mkoani Arusha ambao wamekua katika mgogoro wa ardhi kwa
muda mrefu hali iliyowalazimu kugawanyika katika makundi mawili
yasiyoelewana, Waziri Lukuvi amefafanua kuwa mwenye mamlaka ya
kumilikisha mtu ardhi zaidi ya hekari 50 ni Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania pekee.
“Afisa
huyu wa ardhi ambaye japo hapo awali mlishawahi kumsimamisha kazi kwa
makosa mengune kama haya, lakini kwa sasa makosa haya ni makubwa sana
na sasa afukuzwe kazi, haiwezekani amilikishe hekari zaidi ya 1,500
kinyume na sheria” Alisema Mhe. Lukuvi.
Katika
hatua nyingine Waziri Lukuvi amezifuta hati zote za kimila zilizotolewa
na afisa ardhi huyo kwasababu zimetolewa kinyume na utaratibu kwa
mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999 ambayo hairuhusu kutoa
hatimiliki za kimila zaidi ya hekari 50 bila idhini ya Rais.
Miongoni
mwa watu waliomilikishwa maeneo makubwa kubwa katika kijiji cha
Engarooji wilayani Monduli ni Paulo Ndari mwenye hekari 716, Lekashu
Ng’ene mwenye hekari 301 na Salimu Orkoskos mwenye hekari 268 ambazo
zote pamoja na nyingine Waziri Lukuvi amezifuta.
No comments:
Post a Comment