KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 15, 2014

TANZANIA YAUNGANA NA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUADHIMISHA SIKU YA HIFADHI YA TABAKA LA OZONI


Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Mahenge akiongea na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni linatakalofanyika 16 Septemba, 2014.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakifauatilia kwa makini maelezo toka kwa Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Mahenge yakiyohusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni linatakalofanyika 16 Septemba, 2014.


Na Mwandishi wetu-Dodoma.
Tarehe 16 Septemba, mwaka huu Tanzania itaungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika azimio lake la 49/114 la tarehe 19 Desemba, 1994.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Mwandisi Dkt. Binilith Mahenge wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari 15 Septemba, 2014 kwa lengo la kuongelea juu ya Maadhimisho hayo linalofanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu.
Mwandisi Mahenge ameeleza kuwa tarehe hiyo ni kumbukumbu ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol-1987) kuhusu kemikali zinazomonyoa Tabaka la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka hilo.
Ameendelea kwa kusema kuwa Mkataba huo umepata mafanikio makubwa ya kupunguza zaidi ya asilimia 98% ambapo ni takribani tani milioni 1.8 ya uzalishaji na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni.
“Punguzo hilo limechangia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwasababu baadhi ya kemikali zinamong’onyoa tabaka la ozoni pia husababisha kuongezeka kwa joto duniani”, alisema Dkt. Mahenge.
Akizungumzia kuhusu mikakati ya kitaifa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Mkataba huo, Dkt. Mahenge alisema kuwa 1996 Serikali iliandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni, mikakati hiyo ni pamoja kujenga uwezo wa Taasisi zinazosimamia utekelezaji wa Mkataba, kuweka takwimu za kemikali hizo, kutoa elimu kwa wadau na kwa umma kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili, kusambaza habari kuhusu kemikali na teknolojia mbadala na mikakati mingineyo.
“Hatua hizi zimewezesha Tanzania kuondosha kemikali hizi kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na Mkataba”, alisema Mhe. Mwandisi Mahenge.
Chini ya Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu, serikali iliandaa Mpango wa Usimamizi wa Vipodozi yaani (Refrigerant Management Plan) na katika utekelezaji wake, mambo kadhaa yamefanyika ikiwemo kuandaa Kanuni za Usimamizi wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la hewa ya Ozoni ambazo zilianza kutumika tarehe 7 Desemba mwaka 2007, kusambaza kwa Vitambuzi vya kemikali hizo vipatavyo 18 kwa ajili ya vituo vilivyo mipakani mwa Tanzania, pia kusambaza mitambo na zana za kuhudumia majokofu na viyoyozi kama vile mashine za kunasa na kurejeleza gesi chakavu kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya fani ya kuhudumia majokofu na viyoyozi hapa nchini.
Aliongeza kuwa hadi sasa, Tanzania imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86% ya kiasi cha matumizi ya kemikali hizo, mwaka 1999.
Hapa nchini maadhimisho haya yatafanyika kwa njia ya uelimishaji umma kuhusu Tabaka la Ozoni, faida zake, madhara ya kuharibika kwa Tabaka hilo na matumizi salama ya bidhaa zenye kemikali rafiki kwa tabaka la ozone.
-MWISHO-


No comments:

Post a Comment