Ndugu Filbert Bayi, Katibu wa TOC
Rais wa Kamati ya Olimpiki
Tanzania (TOC), Gulam Rashid, kesho (Oktoba 24 mwaka huu), atafunga kozi ya
makocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Hafla ya ufungaji kozi hiyo
iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na
kuandaliwa na TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itafanyika saa 5 asubuhi
kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kozi hiyo ya wiki mbili iliyoanza
Oktoba 12 mwaka huu, iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli.
Makocha walioshiriki kozi hiyo ni
Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir
Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe
(Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga),
Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid(Geita).
Wengine ni Edna Lema (Morogoro),
George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma),
Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA),
Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil
(Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).
Pia wapo Mohamed Ismail Laiser
(Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas
Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA),
Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho
(Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).
Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa vyeti vya ushiriki tu.
No comments:
Post a Comment