KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 27, 2014

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT. TITUS MLENGEYA KAMANI (Mb) AZINDUA MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI NDANI YA ZIWA VICTORIA, KITEULE CHA BULAMBA WILAYA YA BUNDA, TAREHE 24 NOVEMBA, 2014

Displaying IMG_2172.JPG
Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.
Displaying IMG_2222.JPG
Picha ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao wamepiga hatua kubwa .



Displaying IMG_2271.JPG
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),  Mratibu Mwandamizi wa Mradi Bw. Nehemia Murusuri (wa kwanza kulia) pamoja na Mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mratibu wa Mradi wa Kuondoa Umaskini, Kukuza Uchumi na Utunzaji Endelevu wa Mazingira, Bw. Telesphory Kamugisha (wa pili kulia). Wengine ni baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe hizo.

Displaying IMG_2274.JPG
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bulamba wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa samaki katika Ziwa Victoria kwa kutumia teknolojia ya vizimba (Cages) ambayo ni teknolojia mpya ndani ya nchi yetu.             
Displaying IMG_2253.JPG
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (mwenye Kaundasuti nyeusi) akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya asili mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.                                   

No comments:

Post a Comment