| .Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua jambo kuhusiana na mshindi wa
shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa
na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge
aliibuka na ushindi wa kitita hicho katika droo ya 14 iliyochezeshwa
jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha
Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na Afisa wa
kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa
kutuma neno Jay kwenda 15544. Mkazi wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Uwezo Magendenye (22) , leo ameibuka mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 katika droo ya kumi na nne ya promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Magedenge
binti mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mhudumu wa mapokezi katika
nyumba ya wageni ya Luganga Lodge iliyopo wilayani Kilolo amesema
kuwa amepokea taarifa hizi kwa furaha akiwa kazini na amefurahia
ushindi huu ambao anaamini utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.
“Katika
maisha yangu nimeishapitia mambo mengi nahangaika na maisha hadi
kufikia hapa nilipo nikiwa mhudumu kwenye nyumba ya wageni.Kwa ushindi
huu naamini nitafungua shughuli zangu za biashara ikiwemo kuanzisha
biashara ya maduka ya M-Pesa pia kufungua nyumba yangu ya kulala
wageni na kusaidia ndugu zangu ambao wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali za maisha”.Alisema
“.Nashukuru
Vodacom kwa kuleta promosheni hii ambayo naamini itabadilisha maisha
yangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na kusikiliza
sala zangu .
Aliongeza
kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye promosheni mbalimbali na
hajawahi kufanikiwa kwa ushindi huu anaamini kuwa promosheni
hizi hususani za Vodacom ni za kweli na amewataka wateja wote
kushiriki ili kutopoteza bahati zao za kujishindia mamilioni ya fedha na
kubadilisha maisha yao.
Akiongea
muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom
Tanzania,Rene Meza amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja
wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY
kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema
kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544
iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha
anakatwa shilingi 300/-
Naye
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania alisema kuwa tangu
promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja 2
wamekwishajishindia
milioni 10 na wateja watano wameishajishindia shilingi milioni moja
kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.
“Promosheni
hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya kumi na nne
hivyo bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa
kufanya ni kuhakikisha
kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo
ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544. |
January 29, 2015
BINTI WA MIAKA 22 ASHINDA MILIONI 100 ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment