KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 29, 2015

SITTA ATAKA WADOKOZI BANDARI WASIPEWE DHAMANA

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akizungumza wakati wa ziara ya kikazi  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)  Dar es Salaam jana, baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi. Kalia ni Mkurugenzi Mkuu wa (TPA) Mhandisi Madeni Kipande. Picha na Venance Nestory
 Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema angependa kuona sheria inayataja makosa ya udokozi bandarini kama ya uhujumu wa uchumi ili watuhumiwa wanapokamatwa na kushtakiwa wasipewa dhamana.
Waziri Sitta alisema hayo jana wakati akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), katika mfululizo wa ziara zake kwa mashirika, taasisi na mamlaka zilizo chini ya wizara yake kwa lengo la kufahamiana na kujua changamoto na kupanga mikakati yake katika utendaji.
Akizungumza katika mkutano na watendaji TPA, baada ya kusikiliza taarifa ya utendaji kazi iliyohusisha mikakati, mafanikio na changamoto za mamlaka hiyo, Sitta alisema duniani kote bandari ni kitovu cha uchumi wa nchi.
Alisema vitendo vyovyote vya udokozi na hujuma vinavyofanywa na watumishi wasio waaminifu ni kuhujumu uchumi wa Taifa, hivyo angependa kuona wahusika wanashtakiwa na kunyimwa dhamana.MWANANCHI

No comments:

Post a Comment