KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 29, 2015

LIPUMBA APANDISHWA KIZIMBANI

 
 Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kushawishi wafuasi wake kutenda kosa la jinai.
Wakimsomea shtaka linalomkabili, mawakili wa Serikali Joseph Maugo na Hellen Moshi walidai jana kuwa kati ya Januari 22 na 27 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam aliwashawishi wafuasi wake kutenda kosa hilo kinyume cha sheria.
Baada ya kusomewa, Profesa Lipumba ambaye anatetewa na mawakili; Mohammed Tibanyendera, Peter Kibatala, Hashimu Mziray, Fred Kiwelu na John Malya alikana shtaka hilo na kudai kuwa ni la uongo.
Upande wa mashtaka uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi haujakamilika na kuiomba ipange tarehe nyingine.
Mawakili hao wa Profesa Lipumba waliiomba Mahakama impatie mteja wao masharti ya dhamana yenye nafuu. Hakimu Mfawidhi, Isaya Arufani alimtaka Profesa Lipumba kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika kila mmoja akiwa na barua na kitambulisho kila mmoja kusaini hati ya dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh2 milioni.
Profesa Lipumba alikamilisha masharti hayo na kuachiwa huru saa 9:42 alasiri. MWANANCHI

No comments:

Post a Comment