KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 29, 2015

CILT WAANDAA MKUTANO MKUBWA ARUSHA,MWAKYEMBE AUBARIKI

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa afriKa Mashariki Mh. Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau mbalimbali walijitokeza katika hafla hiyo ya kutafuta fedha za kuendesha mkutano huo utakao fanyika mapema mwezi wa tatu.
Taasisi ya kimataifa ya uhudumiaji wa bidhaa na uchukuzi wa bidhaa CILT yani The Chartered Institute of Logistic and Transport tawi la Tanzania imeandaa mkutano huo mkubwa nchini ambao utafanyika katika mkoa wa Arusha tarehe 3 na 4 mwezi wa Machi lengo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maswala ya usafirishaji na uchukuzi kujadili changamoto mbalimbli katika sekta hiyo.

Mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania George Makuke akizungumza kuhusu mkutano huo na taasisi hiyo inavyofanya kazi. Mkutano huo ambao utafanyika katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha una mipango pia ya kuwakutanisha wanataaluma wa maswala ya uchukuzi na usafirishaji wa bidhaa ili kubadilishana uzoefu katika taluma hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu Zakaria Hanspope akizungumza katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment