![]() |
| Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Makamu wa Pili wa Rais-Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd wakitazama shughuli mbalimbali za vijana wa Mafunzo ya Amali katika fani ya ushonaji. |
![]() |
| Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani wa pili kushoto na Mbunge wa Jimbo la Donge,Mh.Sadifa Juma Khamis wakikabidhi mifuko ya saruji kwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya msingi ya Donge Mtambini,Bwa.Bakari Ame Hussein,Jumla ya mifuko 50 ya saruji ilitolewa na Mbunge Sadifa kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa skuli hiyo. |
![]() |
| Katibu Mkuu Ndugu Kinana sambamba na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Ujumbe wake ukipokelewa na vijana wa CCM jimbo la Donge wakiongozwa na Mbunge wao Mh.Sadifa Juma Khamis,mapema leo alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za CCM-Donge Mtambalike wilaya ya Kaskazini B.Katibu Mkuu Ndugu Kinana yupo katika ziara ya Visiwa vya Unguja na Pemba-Zanzibar akihimiza Uhai wa chama cha CCM na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 |
![]() |
| Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Taifa (UVCCM) ,Mh.Sadifa Juma Khamis akimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pichani kati mara baada ya kuwasili katika jimbo hilo Wilaya ya Kaskazini B,mkoa wa Kaskazini B Unguja kwa ziara ya siku moja.Ndugu Kinana aliwasili katika ofisi za CCM Donge Mtambalike na kupokea taarifa ya chama ya wilaya na utekelezaji wa Ilani,na pia alizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya. |
![]() |
| Mtunza fedha wa kikundi cha ushiriki cha akina Mama ,Saccos (kukopa na kuweka),Bi Mwatime Juma Omar akitoa ufafanuzi mfupi kuhusiana na ushirika huo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana. |







No comments:
Post a Comment