![]() |
| Na Kadama Malunde, Shinyanga
KATIKA hali ya kushangaza, bibi kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa
miaka (70), asiyejulikana jina wala makazi yake, ameanguka akiwa uchi wa
mnyama nyumbani kwa Suzana Mwandu, mkazi wa Mtaa wa Mageuzi mkoani
Shinyanga. Tukio hilo lilitokea juzi ambapo bibi huyo baada ya kuanguka alianza kutembelea makalio bila kuzungumza chochote jambo ambalo limedaiwa ni ushirikina. Akielezea tukio hilo jana, Mwandu alisema lilitokea nje ya nyumba ambapo alishangazwa kumkuta kikongwe huyo akiwa amelala huku akiwa uchi wa mnyama. Mwandu alisema baada ya kikongwe huyo kuanguka, alijivuta hadi kwenye jiko lake lililoko nje ya nyumba ambalo lipo wazina baada ya kuanza kumsemesha ndipo akazinduka na kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka, hali ambayo ilimtia wasiwasi na kutoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya Mtaa. “Nyumba yangu nimeizindika vilivyo, hivyo kikongwe huyu alipokuwa katika safari zake na kupita maeneo ya nyumbani kwangu ndipo akakutana na balaa hilo na hatimaye akajikuta ameanguka na kuingia jikoni kwa ajili ya kujificha. “Unajua siku zote mchawi anapoanguka na ukimwacha kwa muda mrefu bila ya kumsemesha, anaweza kupoteza maisha, hivyo kutokana na mimi kutokuwa na ubaya naye, nikaona bora nimsemeshe ili kumwokoa na baada ya hapo nikampa nguo za kujistiri na aibu ya kuwa mtupu,” alisema Mwandu. Kwa upande wao mashuhuda wa tukio hilo, walidai kuwa bibi huyo huenda akawa ni mchawi kutokana na kauli zake tatanishi alizokuwa akizitoa huku mikono yake ikionekana kukatwa kwa mapanga na kuota sugu.MTANZANIA |
January 31, 2015
TEKNOLOJIA! BIBI KIZEE AANGUKA AKIWA ANASAFIRI ANGANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment