KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 30, 2015

WAFUASI 29 WA CUF WAACHIWA KWA DHAMANA

http://api.ning.com/files/yKWLMefqYBwbFkDtK-9r8JWUXvppD9V4qgdO-7UQkGAYQanjXHCShVlsl-NxBEk*yJhIe7CFK4JFBAf3Ck*-dTOWxHWKuBZA/lipumba.JPG
WAFUASI 29 kati ya 30 waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam wameachiwa leo baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Wafuasi hao walikamatwa majuzi huko Mtoni Mtongani, Dar wakati Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akielekea Mbagala kuwataka wananchi watawanyike baada ya maandamano ya chama hicho kuzuiliwa na jeshi la polisi. Wafuasi hao 29 wameachiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kila mmoja wao kutimiza masharti ya dhamana kwa kutoa kiasi cha shilingi 100,000 pamoja na barua ya mdhamini mmoja ambaye hana hatia.

No comments:

Post a Comment