
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi.
Na Andrew Chale wa modewjiblog
Mshindi wa Januari 2015 wa shindano la wazo la biashara 3N
anatarajiwa kutangazwa siku ya Alhamisi ya Februari 12 kuanzia saa
tano asubuhi jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Dk. Reginald Mengi kupitia kurasa wake wa twitter,
alitangazia umma kuwa Shindano hilo jipya lijulikanalo kwa kifupi -3N,
ikiwa ni kifupisho cha ‘Nitabuni wazo la biashara, Nitatekeleza, na
Nitafanikiwa’, ambapo mshindi wa kwanza wa mwezi Januari anatarajiwa
kutangazwa siku hiyo ya alhamisi Februari 12.
Dk. Mengi aliweka ujumbe huo twittter : “Kutokana na sababu
zisizozuilika mshindi wa Januari wa shindano la 3N atatangazwa Februari
12 saa 5 asubuhi. Samahani kwa usumbufu wowote”.
Kwa mujibu wa Dk. Mengi awali mshind I alitakiwa kutangazwa Jumatano
ya leo ya Februari 11, kabla ya kusogeza mbele hiyo Februari 12.
Shindano hilo litakuwa linafanyika kila mwezi kwa muda wa miezi sita
kuanzia Januari Mosi 2015, hadi Juni 30, 2015, na mshindi wa kila mwezi
atajishindia ruzuku ya shilingi milioni 10 atakazozitumia kutekeleza kwa
vitendo wazo lake la biashara.
Shindano hilo, linawashirikisha Watanzania pekee, litaendeshwa kwa
njia ya mtandao wa kompyuta ambapo mshiriki atatuma wazo lake la
biashara kwa anuani ya twita @regmengi Shindano la Wazo la Biashara.
Katika mchujo wa kwanza jopo la wataalamu litateua mawazo 10 bora Zaidi
na waliotoa mawazo hayo watafanyiwa usaili kwa njia ya simu ili jopo
hilo lijiridhishe kama mawazo waliyoyotuma ni yao binafsi, na kama
wamejipanga vizuri kutekeleza kibiashara.
No comments:
Post a Comment