![]() |
Wanajeshi wa DRC |
Umoja wa mataifa umeondoa usaidizi
wake katika mpango wa kuwashambulia waasi mashariki mwa DR Congo baada
ya serikali kukataa kuwafuta kazi majenerali wawili,msemaji wake
amesema.
Vikosi vya umoja wa mataifa havikuweza kujiunga katika
mashambulizi kwa kuwa majenerali hao wanatuhumiwa na unyanyasaji wa haki
za binaadamu,aliongezea.
Mpango huo wa mashambulizi ulilenga kuwapokonya silaha waasi wa FDLR ambao wanaonekana kama tishio la uthabiti wa eneo hili.
Serikali ya DR Congo haijatoa tamko lolote kuhusu hatua hiyo ya umoja wa mataifa.
Awali
serikali hiyo ilisema kuwa iliwachagua wanajeshi wake hodari kupigana
na FDLR,hivyobasi haitachukua amri kutoka kwa umoja wa mataifa.BBC
No comments:
Post a Comment