![]() |
| Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Abraham Mengi akiongea maneno ya kuapa na kumvisha pete ya ndoa Miss Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe 'K-Lynn' wakati wakifunga ndoa. |
![]() |
| Mengi akimkumbatia K-Lynn kama ishara ya upendo. |
![]() |
| Maharusi wakipiga picha ya pamoja. Wa pili kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania na Miss World Africa 2005) na mumewe Luca ambaye pia ni mmiliki wa mtandao wa Bongo5. |
![]() |
| Maharusi na wapampe wao wakitembea ufukweni sambamba na watoto wao mapacha. |
![]() |
| ....wakirusha maua na kufurahia. |
MISS Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe ameacha historia ya
aina yake nchini, baada ya kufunga ndoa na Mwenyekiti Mtendaji wa
makampuni ya IPP, Dk. Reginald Abraham Mengi, tukio lililofanyika nchini
Mauritius mwishoni mwa mwezi uliopita.
Jack, ambaye pia anafahamika kwa jina lake la kisanii kama K- Lynn,
anaacha historia hiyo nchini Tanzania kwani licha ya kufunga ndoa hiyo
akiwa tayari na watoto wawili mapacha aliozaa na mumewe, pia ndiye
mshindi wa kwanza wa shindano hilo kubwa, kuolewa na bilionea baada ya
kuwa katika uhusiano kwa miaka kadhaa pasipokuwa na kashfa na miezi
minne baada ya kuvalishwa rasmi pete ya uchumba.
K-Lynn ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, anaweka pia
historia hiyo kwa kuolewa na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa na wenye
kuheshimika katika Afrika Mashariki, ambaye licha ya kumiliki vyombo
vikubwa vya habari vikiwemo redio, magazeti na televisheni, pia ni
mmiliki wa viwanda, migodi ya madini na biashara nyinginezo kubwa. IPP
inamiliki vituo vya Radio One, Capital Radio, East Africa Radio, ITV,
Eatv, Capital TV na magazeti la Nipashe, The Guardian na mengine kadhaa.
Harusi yao inayotajwa kuwa ni moja kati ya ndoa za kifahari nchini
Tanzania, ilihudhuriwa na idadi ndogo ya watu wapatao 50, ambao ni ndugu
wa karibu wa familia hizo mbili, pamoja na marafiki muhimu wa pande
zote mbili.
Mengi, anayetajwa kuwa tajiri wa tatu nchini, miezi minne iliyopita,
alimvalisha pete ya mchumba msanii huyo aliyekuwa na uwezo mkubwa wa
kufanya muziki, wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa
iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na watu wachache.
Baadhi ya washindi wengine wa shindano la Miss Tanzania walioolewa ni
pamoja na Hoyce Temu (1999), Miriam Magese (2001) Faraja Kota (2004),
Nancy Sumari (2005) na Sarah Israel (2011).
STORI: OJUKU ABRAHAM/GPL. PICHA: BONGO5







No comments:
Post a Comment