![]() |
| Mkurugenzi
wa Masoko na Uhusiano UTT-AMIS, Daud Mbaga (aliyesimama kushoto),
akitoa elimu ya uwekezaji wa pamoja kwa wakazi wa Mbeya waliotembelea
maonyesho ya kitaifa ya Biashara kwenye ukumbi wa Mkapa, Soko la Matola.
Swali :Una wito kwa jamii? (Mbaga anajibu)
Jibu: Wito wangu kwa jamii ni wachangamkie uwekezaji huu kwani unatoa
faida nzuri, na usalama wa uwekezaji umezingatiwa, na isitoshe swala zima la
ukwasi limepewa uzito mkubwa. Tuchukue mfano wa kujenga nyumba, kila mtu
anapenda awe na nyumba nyingi na bora. Leo hii viwanja katikakati ya jiji ni
bei sana hivyo ukiwa na shilingi milioni mia moja utajenga nyumba hiyo nje
kidogo ya mji na utaipangisha na kupata fedha kati ya laki tano hadi sita kwa
mwezi .Lakini je ni rahisi kupata fedha hii ya mkupuo?Aghalabu kwa watakaoweza
ni wachache.
Hivyo watumie mifuko hii kuweza fedha zao na kukuza mitaji ili
waweze kufanya uwekezaji kama huo wa kujenga nyumba. Lakini pia mwingine anaweza
wekeza kiasi hicho kwa mkupuo cha shilingi milioni mia moja kwenye
mifuko na kikampatia faida sawa au zaidi ya shilingi laki sita kwa
mwezi, ambapo ni sawa na bei ya
kupangisha nyumba aliyojenga kwa kiasi cha shilingi milioni mia moja hizohizo. Kumbe basi wakati mwingine kupitia mifuko ya
UTT -AMIS unaweza pata faida shindani na kukurahisishia njia mbadala za kupata
kipato. Mfano Mfuko wa Umoja umekuwa
ukikua kwa zaidi ya wastani wa asilimia 30 kwa kila mwaka tokea uanzishwe mwaka
2005
|
April 9, 2015
KUTOKA UTT-AMIS: KUMBE UNAWEZA UKAWEKEZA FEDHA ZAKO UTT-AMIS NA UKAISHI KAMA BABA MWENYE NYUMBA JIJINI!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment