![]() |
| Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vikundi hivyo. |
![]() |
| Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akikabidhi msaada
wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto wa kituo cha kulea watoto
yatima cha Malaika kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, Dar es
Salaam jana.
…………………………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU,
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amekabidhi msaada
wa vyakula na vitu mbalimbali vyenya thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa
vikundi vitatu vya kulea watoto yatima, Dar es Salaam jana kwa ajili ya
kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.
Akikabidhi msaada huo Meya Yusuph
Mwenda aliwataka watanzania kuwa na moyo wa kusaidia watoto hao hususan
katika msimu wa Sikukuu ikiwa ni njia mojawapo ya kuwafariji watoto hao.
“Hakuna anayependa kuona watoto
hawa wanaongezeka mitaani, Na Serikali inafanya juhudi kubwa kuondoa
tatizo la watoto hawa hasa wanaotelekezwa mitaani lakini peke yake
haiwezi, ni lazima wananchi muunge mkono juhudi hizo.” Alisema Mwenda.
Alisema kuwa badala ya watu
kusherehekea Sikukuu majumbani mwao ni vema wakajumuika na watoto hao
ili kuwafanya nao wajisikie wapo na wazazi wao.
Msaada aliotoa Meya huyo ni pamoja
na Mchele, Sukari, Mafuta, Unga wa Ngano, Unga wa Sembe, Sabuni za
miche na unga, Mbuzi na vitu vingine.
|




No comments:
Post a Comment