KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 29, 2015

RAIS BUHARI AAPISHWA

Embedded image permalink
Kerry akiwasili kwenye sherehe hiyo
Abuja, Nigeria (CNN) Rais wa Nigeria ameapishwa leo katika sherehe iliyomaanisha mabadiliko ya uongozi kwa amani baina vyama hasimu vya siasa.

Muhammadu Buhari, aliyeshinda uchaguzi mwezi Machi, ameapishwa leo katika Mji Mkuu wa Abuja . Nje ya Uwanja kulikuwa na vikundi mbalimbali vya sanaa vikitumbuiza

Umati wa watu ulishangilia huku wengi wakiwa wameshika mafagio, kauli mbiu ya Rais huyo ilikuwa ni' fagio jipya'.

"Nawashukuru wote kwa upendo wenu katika kipindi cha kampeni, alituma ujumbe wa twita na kusema" Katika Ujumbe wake wa Twita aliandika" Mimi ni wa  kila mtu, lakini si wa mtu,".

Buhari amechukua madaraka kutoka kwa Goodluck Jonathan,akirithi taifa linalokabiliana na waasi wa Boko Haram, pamoja na ukosefu wa mafuta kutoka katika nchi yenye hazina kubwa ya mafuta Duniani

Waziri wa Mamo ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry aliungana na  viongozi wengine duniani kwenye hafla hiyo.

"Nina furaha kurudi Nigeria na kupewa heshima ya kuongoza Marekani katika hafla hii,"

Zuma alisema safari yake ni fursa ya kujadiliana juu ya ushirikiano baina ya Nigeria na Afrika Kusini mataifa yenye nguvu barani Afrika.

"Ziara hii ya kikazi, Nigeria inawakilisha fursa muhimu ... kujadili masuala ya kimkoa na kimataifa," alisema 

Buhari alitawala kabla.

Buhari aliwahi kuwa kiongozi wa kijeshi Nigeria, katawala Nigeria miaka ya sitini na tisini.

Mapinduzi ya kijeshi yalimweka madarakani mwaka 1983, na yeye alipunduliwa miaka miwili baadaye. Nchi hiyo iliandamwa na mapinduzi mengi ya kijeshi miaka ya nyuma.

Utawala wake ulizingatia nidhamu, wakosoaji wake wanasema ulivunja haki za binadamu.

Kabla ya uchaguzi, mchambuzi wa masula ya Afrika Ayo Johnson, anasema  wapiga kura walimchagua kutokana na wasifu wake na walitaka mtu wa kupambana na Boko Haram.

"Wananchi wengi, wanamkumbuka kama kiongozi wa kijeshi, enzi za udikteta, wanataka mtu wa kupambana na ugaidi,"

Mwaka huu peke yake, magaidi wameua raia 1,000 , zaidi kutoka eneo la Kaskazini.

'Kuzaliwa upya Kidemokrasia'

Ugaidi, rushwa na uchumi ni vipaumbele vya utawala huo mpya.

Wasanii wakiwatumbuiza wageni
Msanii akinasa kumbukumbu ya leo
Buhari lipiga kampeni akijiita,"amezaliwa upya kidemokrasia,akisisitiza kuwa usala wa nchi ndicho kipaumbele,"

No comments:

Post a Comment