![]() |
| Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye
Kauli
ya Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape
Nnauye, kudai chama chake kitaendela kuongoza nchi hata kama ni kwa
kura za wizi, chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibuka na
kumjibu kuwa hizo ni ndoto za mchana.
Akizungumza na NIPASHE kwenye ofisi za Chadema Wilaya ya Chato,
Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa (Bavicha), Julius Mwita,
alisema chama chake kipo kwenye maandalizi kamili ya kuingia Ikulu na
kwamba mbinu za CCM kuendelea kuiba kura mwisho wake umefika.
Alisema kila mbinu chafu za CCM zilizoandaliwa kuhujumu Uchaguzi
Mkuu wa mwaka huu zimeshabainika ikiwamo kuagiza magari 700 ya kutawanya
wananchi kwa maji ya kuwasha, badala ya kujikita kubuni mbinu bora za
kudhibiti mauaji ya walemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe
wanaouawa bila hatia.
"Nikuhakikishie kuwa mwaka huu Chadema kupitia Ukawa tunaingia
madarakani...hivi sasa CCM wanaweweseka tu wasijue la kufanya ndiyo
maana wamekuwa na foleni kubwa ya wagombea urais kana kwamba ni taasisi
ya kuchezewa hadi na wasomi wa darasa la saba," alisema.
Alisema tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu imejionyesha kwenye
uchaguzi mdogo uliomalizika ambapo Ukawa ulikishusha CCM katika viwango
vya ushindi kutoka aslimia 95 hadi kufikia asilimia 64 na kwamba hatua
hiyo ni wazi kwamba Ukawa wanakwenda kuchukua dola.
Akizungumza hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara wilayani Chato
mkoani Geita, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdurahman Kinana, aliwataka
wafuasi wa chama hicho kuikosoa serikali ya CCM inapofanya mambo
yasiyopaswa na ikiwezekana wafanye maandamano kupinga badala ya kusifia
kila kitu.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida Nnauye, alisisitiza
kuwa CCM kitaendelea kuongoza nchi kwa kuwa ni chama makini na kwamba
hata kama itakuwa kwa kura za kuiba na kudai kuwa bao ni bao hata kama
ni la kidole iwapo kama mwamuzi hataweza kuona.
Kauli ya Nape ilipokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wananchi
waliohudhuria mkutano huo huku wakidai ameamua kutoa siri inayowafanya
CCM kupata ushindi katika chaguzi zilizopita huku wengine wakisifia kuwa
ni wakongwe wa siasa na kwamba mbinu zote za ushindi wanazo.
CHANZO:
NIPASHE
|
June 20, 2015
CHADEMA: NAPE ANAOTA NDOTO ZA MCHANA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment