| Pichani ni Mhudumu wa Mapango ya
Chinhoyi Cephas Sithole akitoa maelezo kwa timu ya waandishi wa habari
waliombatana na wadau wa utalii kutoka nchini Afrika Kusini kwenye
ziara hiyo ya kutembelea vivutio vya utalii nchini Zimbabwe katika
mapango Chinhoyi.(Picha zote na Zainul Mzige). Na Modewjiblog team, Harare Waandishi wa habari kutoka vyombo 5 vya habari vya magazeti ya Tanzania ikiwemo mtandao wa habari wa modewjiblog ambao ni Justin Damiana (The African), Frank Aman (The Guardian), Zainul Mzige (modewjiblog), Mariam Said (Daily News) pamoja na Timothy Kitundu (East Africa Business Week) walipata mwaliko kutoka Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA) kufanya utalii katika mapango ya Chinhoyi, Ziwa Kariba, Shamba la ufagaji wa Mamba, Hifadhi ya Taifa ya Kariba, Bandari ya Zambezi pamoja na ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe. Safari ya kuelekea nchini Zimbabwe ilidhaminiwa na Shirika la usafiri wa Anga wenye gharama nafuu Fastjet Tanzania ikiwa ni moja ya mipango yao ya kuimarisha safari zake za kutoka Dar es Salaam-Lusaka na Harare. Safari hiyo ilikuwa maalum kwa ajili kuhudhuria maonyesho ya naneya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) ambayo yameanza kurindima jijini Harare katika ukumbi wa Harare International Conference Centre (HICC). |
| Waandishi wa habari kutoka Tanzania waliosafirishwa na Shirika la ndege lenye gharama nafuu nchini Fastjet kuhudhuria maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Shanganai yanayoendelea nchini Zimbabwe. Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu (East Africa Business Week), Mariam Said (Daily News) pamoja na Justin Damiana (The African) wakiwa wameketi kwenye mapango ya Chinhoyi huku wakibadilishana mawazo na wadau wa utalii kutoka Afrika Kusini. |
| Kundi jingine likiwa kwenye ziara ya ziwa Kariba likiongozwa na Rumbidzai Mudzengerere wa Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA). |


No comments:
Post a Comment