| Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye |
Kazi ya
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ya kusaka wadhamini juzi nusura
iingie dosari baada ya wanachama kutaka kuchana fomu zenye orodha ya
wadhamini kwa madai kuwa hawakupewa “nauli” ya kwenda ofisi za CCM
kufanya kazi hiyo.
Wakati
tafrani hiyo ikitokea mjini Mbeya, Balozi Amina Salum Ali alisema mjini
Tanga kuwa hajawahi kuona nchi ambayo mtu anaiba fedha, halafu anaambiwa
azirejeshe bila ya kuchukuliwa hatua zozote, akisema huo ni udhaifu
mkubwa katika kudhibiti ufisadi.
Katika
sakata la Mbeya, kundi la baadhi ya wanachama kutoka kata nne
waliokabidhi kadi na kuandikwa majina yao kwenye ofisi za CCM za Wilaya
ya Mbeya Mjini, liliambiwa kuwa hakukuwapo na posho kwa ajili ya kazi
hiyo.
Kauli hiyo ilisababisha wanachama hao kupora na kutaka kuchana fomu iliyokuwa na majina yao.
Katibu wa
CCM wilaya hiyo, Kulwa Milonge alisema tukio hilo lilikuwa kubwa na
kuhatarisha usalama, lakini chama kiliingilia kati na kusawazisha mambo.
Milonge alisema hadi mwisho wa tukio hilo, ofisa aliyetumwa na Sumaye kukusanya saini hizo aliondoka na majina 45 ya wadhamini.


No comments:
Post a Comment