![]() |
MCHEZAJI
mpya anayefanya majaribio kwa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga,
Lansana Kamara amefuzu majaribio hayo baada ya uongozi wa Yanga
kuridhishwa na kiwango chake.
Ni wiki
moja imepita tangu mchezaji huyo ajiunge kwenye mazoezi ya Yanga
akifanya majaribio na kikosi hicho kusaka nafasi ya kusajiliwa msimu
ujao.
Akizungumza
na kituo kimoja cha redio jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha
alisema Kamara ni aina ya mchezaji ambaye Yanga inamhitaji kwani ana
kiwango kizuri kitakachowasaidia kufanya vizuri kwenye michuano
mbalimbali ya kimataifa.
“Kamara
ni mchezaji mzuri na hata Kocha ametueleza kuwa anafaa kwani ana kiwango
kizuri, tunamhitaji na ikiwa mambo yatakuja vizuri hasa katika
kuongezwa idadi ya wachezaji wa kigeni tutamsajili,” alisema Dk Tiboroha
akimzungumzia mchezaji huyo raia wa Sierra Leone.
Dk
Tiboroha alisema kwa sasa wanasubiri tamko la Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kama wataongeza idadi ya usajili wa wachezaji wa kigeni
ndipo wachukue hatua mara moja.
Alisema
iwapo idadi itaongezwa watamsajili mchezaji huyo, lakini ikiwa
hawataongeza, tayari wana wachezaji watano wa kigeni wenye mikataba
labda itokee apunguzwe mmoja na nafasi ichukuliwe na kiungo huyo
aliyeonesha uwezo.
Yanga
inao Amissi Tambwe (Burundi), Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite (Rwanda),
Andrey Countinho (Brazil) na Kpah Sherman (Liberia) katika orodha ya
wachezaji wake watano wageni.
Hivi
karibuni, TFF ilitoa waraka kwa klabu kupendekeza idadi ya wachezaji
kisha Kamati ya Utendaji ikae na kulijadili, agizo ambalo klabu
mbalimbali zilipokea kwa mikono miwili na kuonesha utayari wa ongezeko.
Yanga
tayari walipendekeza idadi ya wachezaji wanane, wakati klabu nyingine
kama Azam FC ilisema idadi yoyote itakayoongezwa watafurahia ili
wasajili wachezaji wenye uwezo watakaowasaidia katika michuano ya
kimataifa.
Kuhusu
maombi ya klabu hizo, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesiga aliliambia
gazeti hili jana kuwa Kamati ya Utendaji inatarajiwa kukutana Jumamosi
ya wiki hii Zanzibar kwa ajili ya kupitia mapendekezo yote.
Alisema
baada ya kikao hicho watatoa tamko lao kama maombi hayo yatapitishwa ama
yatakuwa yamekataliwa kwa kuwa dirisha la usajili limeshafunguliwa na
timu zinasubiri tamko hilo kuchukua hatua. (HABARI LEO)
|
June 17, 2015
KAMARA AFUZU YANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment