| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Siku ya Tabianchi Afrika, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya. Kuongamano hilo lilifanyika jana Juni 17, 2015 kwenye Ukumbi wa Nkhurumah Chuo Kikuu Dar es Salaam, jana. Picha na OMR |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa watafiti wa Kituo cha 'Center For Climate Changes Styles', Khalid Mwakobaa (kulia) na Rdith Benedict, wakati alipotembelea katika Mabanda ya maonesho kwenye Kongamano la Siku ya Tabianchi Afrika, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Nkhurumah Chuo Kikuu Dar es Salaam, jana. Picha na OMR |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa na Mtaalamu
wa uchakataji wa bidhaa za ngozi, Stephano Chifwaguzi, (kulia) wakati alipokuwa
akitembelea mabanda ya maonesho katika Kongamano la Siku ya Tabianchi Afrika,
lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Nchi Wanachama
wa Umoja wa Ulaya, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Nkhurumah Chuo Kikuu Dar es
Salaam, jana. Picha na OMR |
| Picha ya pamoja kwa kumbukumbu, baada ya ufunguzi wa Kongamano hilo. Picha na OMR |


No comments:
Post a Comment