![]() |
| Mshukiwa wa mauaji Storm Roof (21) akiwa ameshikilia karatasi za mahakama. |
![]() |
| Storm Roof akiwa amesindikizwa na polisi kwenye ndege kwa safari ya kurudishwa Carolina Kusini. |
![]() |
| Muuaji wa Watu tisa alionekana anatabasamu baada ya kukamatwa na polisi.
Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la kihistoria mjini Carolina Kusini amekamatwa.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami na bunduki aliketi katika mkutano wa mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja kabla ya kufyatua risasi na kuwaua wanawake sita na wanaume watatu akiwemo mchungaji wa kanisa hilo. Maafisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki. Bi Lynch amesema idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini njia mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa. Vyombo vya habari vya Marekani vinasema kuwa bwana Storm alikamatwa huko Selby Carolina kaskazini saa 13 baada ya shambulizi. Mtu wa karibu wa mshukiwa, Dalton Tyler alisema Roof alikuwa akizungumzia kufanya shambulizi kwa kipindi cha miezi sita mfululizo. "Alikuwa na tabia ya ubaguzi na mambo mengine, alisema ana mpango wa kuanzisha vita kwa kufanya shambulizi na kisha kujiua yeye mwenyewe," Alisema Tyler. Mjomba wa mshukiwa, Carson Cowles alisema mwezi wa nne mwaka huu Roof alipewa Pisto kama zawadi ya sherehe ya kuzaliwa. Alisema licha ya hivyo, familia yao imeshtushwa na tukio hilo lililofanywa na Roof . "Hakuna aliyejua kama hili lingetokea, kama anahusika na atakamatwa ni lazima aadhibishwe kwa kile alichokifanya," alisema. Akiongea kuhusu tukio hilo ikulu jana Rais Barack Obama alilaani kitendo hicho. alisema, kitendo cha mauaji hayo kufanyika katika kanisa la watu weusi linaamsha maswali kuhusu historia mbaya ya ubaguzi wa rangi Marekani. Alisema suala hilo linaashara kuwa kuna umuhimu wa kudhibiti matumizi ya silaha. Chanzo: BBC na Dailymail |





No comments:
Post a Comment