![]() |
| Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda. Makada wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotafuta udhamini katika maeneo mbalimbali ya nchi wamevuna maelfu ya wanachama waliojitokeza kuwadhamini kuomba uteuzi wa kugombea urais wa Tanzania.
Makada hao ni Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowasa; Waziri Mkuu wa
sasa, Mizengo Pinda; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe na Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) katika Umoja wa Mataifa
(UN), Amina Salum Ali.
Lowassa alikuwa mkoani Singida, Pinda mkoani Katavi, Membe na Balozi Amina walikuwa mkoani Tanga.
PINDA APATA 9,141
Pinda amepata wadhamini 9,141 baada ya kuhitimisha udhamini katika mkoa wa Katavi.
Hadi jana mchana alikuwa amekwishapata wadhamini 4,243 kwa kuzuru
vituo viwili tu vya Inyonga na Mpanda Mjini. Lakini hali ilibadilika
alipofika kijijini kwao Kibaoni kwenye ofisi CCM kata ya Kibaoni ambako
alikuta maelfu ya watu wakimsubiri ili wasaini fomu za kumdhamini.
Akitangaza idadi ya watu waliojitokeza kumdhamini Waziri Mkuu,
Katibu wa CCM Wilaya ya Mlele, Sidael Goroi, alisema tarafa za Mpimbwe
na Mamba ambazo ziko kwenye Bonde la Ziwa Rukwa zimetoa wadhamini 3,450
wakati tarafa ya Nsimbo imetoa wadhamini 1,448 na kufanya jumla ya
wadhamini 4,898 kwa juzi jioni tu.
Tarafa ya Mpimbwe ambako Waziri Mkuu anatoka ina kata tisa zikiwamo za Kibaoni, Mwamapuli, Ikuba, Usevya, Mbede na Majimoto.
Katika kituo chake cha kwanza cha Inyonga yalipo makao makuu ya wilaya yake ya Mlele, Waziri Mkuu alipata wadhamini 1,440.
Aliporejea Mpanda mchana alipata wadhamini 2,803 na kufanya jumla ya wadhamini 4,243 kwa vituo hivyo viwili.
Waziri Mkuu aliwashukuru wote waliomdhamini huku akiwaomba
waendelee kumuombea safari zote zilizo mbele yake na zoezi zima liende
vizuri kwani suala la urais siyo lelemama bali ni la kumtanguliza Mungu.
Waziri Mkuu Pinda alisema: “Suala la urais si la kufa na kupona
bali ni la kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwanza. Kila mgombea anapaswa
amuombe Mungu kwamba kama itampendezea na kumuona anafaa ndipo amchague
yeye (mtangaza nia).”
“Ndiyo maana mara zote huwa nawaambia wenzangu kwamba hakuna haja ya kutukanana wala kupakana matope.
Huwa nawaambia tusikwaruzane wala tusitukanane kwa sababu hakuna ajuaye Mwenyezi Mungu amemuandaa nani miongoni mwetu,” alisema.
Aliwataka wananchi na viongozi wa wilaya hiyo watoe ushirikiano kwa wagombea wengine watakaofika wilayani humo kuomba wadhamini.
LOWASSA AVUNA 22,758
Wanachama 22,758 wamejitokeza kumdhamini Lowassa mkoani Singida.
Mkoa wa Singida umevunja rekodi kwa kutoa idadi kubwa ya wadhamini ikilinganishwa na mikoa mingine ambayo ameitembelea.
|
June 17, 2015
PINDA, LOWASSA, MEMBE WAZOA MAELFU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment