![]() |
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,Stephen Wassira
MGOMBEA wa nafasi ya urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Stephen Wassira amesema kujitokeza kwa idadi kubwa ya wanaoomba nafasi
hiyo kwa tiketi ya chama hicho inatokana na ukubwa wa CCM, ambayo ina
hazina kubwa ya viongozi.
Akichangia hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016
bungeni mjini hapa jana kwa kujibu baadhi ya hoja zilizojitokeza wakati
wa mjadala, Wassira ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
alisema CCM ni tofauti na vyama vingine ambavyo idadi ya viongozi wao
wakishapanda helikopta hakuna mwingine anayebaki chini.
Alisema CCM ni chama kikubwa chenye demokrasia na wala wananchi
wasitishwe na idadi kubwa ya wawania urais CCM ambao sasa wanakaribia 40
na kusisitiza kuwa chama hicho kina utaratibu mzuri unaokubalika na
wenye kueleweka kwa jamii kuhusu namna ya kupata viongozi.
“Wingi wa wagombea urais ndani ya CCM unatokana na ukubwa wa chama na
kukubalika kwake, tofauti na vyama vingine ambavyo viongozi wake
wakishapanda helikopta hakuna tena mwingine anayebaki chini,” alisema
Wasira.
Pia alieleza kuwa wakati akiwa katika harakati zake za kusaka
wadhamini alisafiri kwa siku moja kutoka Songea mkoani Ruvuma hadi
Sumbawanga mkoani Rukwa jambo ambalo kwa zamani ilikuwa vigumu na hiyo
ni kazi kubwa ya CCM.
Alisema suala la maendeleo ni mchakato na si jambo la siku moja na
kushangaa wapinzani kukosoa kwa kudhani maendeleo ni kama mvua na
kueleza kuwa baadhi ya mambo yanasemwa na wapinzani sababu huu ni mwaka
wa uchaguzi na kudai yatasikika mengi kipindi hiki.
Alieleza kuwa kura hazipatikani kwa mbunge kusemasema bali
zinapatikana kutokana na mambo mazuri uliyoyafanya kwa wananchi na
kutaja mafanikio mbalimbali ambayo serikali ya Awamu ya Nne chini ya
Rais, Jakaya Kikwete imeyafanya.
|
June 23, 2015
WASSIRA AELEZA SIRI FOLENI YA URAIS CCM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment