![]() |
| Mchungaji Clementa Pinckney aliyeripotiwa kuuawa kutokana na shambulio hilo. |
![]() |
| Waumini wa kanisa la AME na watu wa majirani wa eneo la tukio wakiwa katika majonzi baada ya kutokea shambulio hilo. |
![]() |
| Barabara zikiwa zimefunga kufuatia shambulio lililoua watu tisa kanisani. |
![]() |
| Askari wakiwa katika harakati za kuimarisha ulinzi eneo la tukio. |
![]() |
| Kijana akiwa katika hali ya sintofahamu na huzuni kubwa baada ya watu kufika eneo la tukio na kuuliza kilichotokea. |
![]() | |
| kundi la vijana wakiwa wanasali karibu na eneo la kanisa baada ya tukio la mauaji kutokea.
Carolina Kusini, Marekani
POLISI katika jimbo la Carolina Kusini nchini Marekani
wamesema mtu mmoja aliyekuwa na bunduki amewapiga risasi na kuwaua watu tisa
ndani ya kanisa la Methodist lililoko eneo la Charleston.
Wamesema kwa sasa wanamtafuta mshukiwa huyo anayeaminiwa
kuwa kijana wa Kizungu mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka ishirini.
Shambulio hilo limefanyika ndani ya kanisa la Emmanuel
African Methodist Church maarufu kama AME, kanisa linaloaminika kuwa la zamani
zaidi linalotumiwa na watu wa asili ya Afrika nchini Marekani.
Polisi wamesema kuwa shambulio hilo linatokana na chuki ya ubaguzi wa rangi ambapo pia limehusishwa na nguvu ya kisiasa
kati ya vyama viwili vya siasa katika eneo la Charleston huko South Carolina
kutokana na kile kinachodaiwa kuwa limefanyika saa chache kabla ya Mchungaji
Pinckney kukutana na mwendesha kampeni wa Chama cha Democratic cha Marekani,
Hillary Clinton, katika sehemu ya kampeni ya kuwania urais wa nchi hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo alimtaka mama mmoja
wa makamu kuondoka kanisani hapo kabla hajatekeleza azma yake hiyo ya kufanya
shambulio hilo.
Lengo la kumwondoa mama huyo lilikuwa ni kumfanya aende
akawaambie watu wengine kilichotokea.
Watu wanane walikufa papo hapo na mwingine alifariki akiwa
anapata matibabu hosipitali. Aidha
majeruhi mmoja anayeendelea kupata matibabu ameripotiwa kuwa katika hali nzuri.
Mchungaji Pinckney wa kanisa hilo na Seneta wa Jimbo la
Carolina Kusini, ni miongoni mwa walioripotiwa kuuawa kutokana na shambulio.
Duru za habari kutoka kwa walioshuhudia tukio hilo zinasema
mtoto wa miaka mitano amenusurika kifo kutokana na shambulio hilo baada ya
kuambiwa na bibi yake aliyeambatana naye kanisani kuwa aigize kama amekufa mara
tu shambulio lilipoanza.
Chanzo: BBC na Dailymail
|








No comments:
Post a Comment