![]() |
| Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba.
Enzi za uhai wake.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt.
Fenella Mukangara (Mb.) alituma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu
Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa
Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni
15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.
Katika salamu hizo, Mhe. Mukangara alisema kuwa ni jambo la kusikitisha
kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika
kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Waziri huyo aliongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole , unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake.
Alisema, amepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu
wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi
anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika
kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja.
“Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu. “Kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao, napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina,” Alisema Waziri Mukangara |
June 15, 2015
WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO YATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH MKUU WA TANZANIA MUFTI SHAABAN ISSA BIN SIMBA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment