Maofisa
wa usalama barabarani wakichukua taarifa eneo la ajali.
|
Coaster
baada ya kuigonga treni.
|
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.
WATU watano wamepoteza maisha huku
24 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria kuligonga treni lililokuwa linatoka
Morogoro – Dodoma leo asubuhi katika eneo la Kibaoni, wilayani Kilosa mkoani
Morogoro.
Basi lililohusika katika ajali hiyo
ni aina ya Isuzu Coaster lenye namba za usajili T837 CTM linalomilikiwa na
Feisal A. Khuwel wa wilayani Kilosa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ajali hiyo imetokea leo
majira ya saa 1 asubuhi na imetokana na uzembe wa dereva wa basi.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wiaya
Kilosa, Dickson Masale
amethibitisha kupokea miili ya watu watano akiwemo
dereva wa basi pamoja na majeruhi 24.
Source; Sophiembeyu blog.
|
No comments:
Post a Comment