Na Benjamin Sawe,Maelezo
Mabadiliko
katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini yamepelekea kuwepo na
mabadiliko ya sheria ya mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF).
Sheria ya Mfuko wa pensheni wa PSPF sasa inaruhusu kusajili wanachama
katika sekta zote za umma na binafsi. Na kwa sasa mfuko una mipango
miwili ya uchangiaji wa lazima yaani PSPF Mandatory Scheme na mpango wa
uchangiaji wa hiari yaani PSPF Supplementary Scheme
Akizungumza
katika mahojiano maalum na Mwandishi wa Makala hayaBi Mwanjaa Sembe,
Meneja Mpangowa Uchangiaji wa Hiari PSPF anasema uwasilishaji michango
kwa kutumia huduma ya MaxMalipo itawasaidia wachangiaji kupata huduma za
michango yao.
Anasema
huduma ya kulipia kupitia mfumo wa Maxmalipo imeanzishwa na mfuko wa
pensheni wa PSPF kwa ajili ya kupanua wigo kwa wanachama wa mfuko huo
kuchangia na kujua salio la michango yao popote walipo ambapo huduma
hiyo itawarahisishia watumiaji kutosafiri kwa umbali mrefu ili kupata
huduma hiyo.
Mfuko
umeona adha na shida walizokuwa wanazipata wateja wetu ndio maana
tukaamua pamoja na huduma nyingine zitolewazo na mfuko wetu tujiunge na
wenzetu wa Kampuni ya MaxCom inayotoa huduma ya Max Malipo ili kuweza
kuwakomboa wateja waweze kuchangia pamoja na kujua kiasi cha michango
yao kwa urahisi kwa kutumia huduma hiyo hivyo kuwafanya kuwa na muda
mrefu wa kutafuta kipato badala ya kusafiri kwa umbali mrefu kufuata
huduma.Anasema Bi. Sembe.
Anasema
masuala ya hifadhi ya jamii yanagusa kiini muhimu sana cha wafanyakazi
kwenye sekta rasmi na sekta zisizo rasmi hasa za watu masikini pamoja na
sekta ya bima za jumuiya za waajiri.
Uchunguzi
unaonyesha kuwaIdadi kubwa ya watu waliomo katika mifuko hii ya hifadhi
ya jamii ni wale ambao wameajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi. Hifadhi ya
jamii ni haki ya kila mtu ndiyo maana mfuko wa pensheni wa PSPF wana
mpango wa uanachama wa hiari kama mkakati wa makusudi juu ya kupanua
wigo wa hifadhi ya jamii ili kuhakikisha ya kuwa hata wale waliojiajiri
kujiunga na mfuko wa PSPF na hata wale wanachama wa mifuko mingine
iliyopo kuweza kuweka akiba ya ziada.
No comments:
Post a Comment