Na Mwandishi Wetu
..………………
Kama sehemu ya
mkakati wake wa kusaidia utoaji wa mafunzo kwa maafisa wa viwanja vya
ndege,kampuni ya Fastjet Tanzania imeingia katika makubaliano na kampuni
inayojihusisha na wanyamapori ya Uholanzi ijulikanayo kama AviAssist ambayo itatoa mafunzo kuhusu namna ya ulinzi wa wanyamapori kwa maafisa wa viwanja vya ndege.
Akizungumza na vyombo vya habari, Meneja mkuu wa kampuni ya Fastjet ukanda wa Afrika mashariki Jimmy Kibati
alisema kuwa, Fastjet itaendasha mafunzo haya katika ofisi zake za
makao makuu jijini Dar es Salaam, huku akiongeza kwamba kozi itabeba
sehemu ya wadau wote ambao uelewa na ushirikiano wao ni muhimu kwa
utekelezaji kwa vitendo mpango wa usimamizi wa wanyamapori kwenye
viwanja vya ndege.
Mafunzo yatafuata mwongozo wa kimataifa kwa muundo wake kutoka kwa
mashirika ya ndege ya kimataifa na wadhibiti wakuu kama vile shirikisho
la utawala la safari za anga marekani ,” alibainisha Kibati.
Wakati wa
kutangazwa kwa mkataba, ilionyeshwa kwamba licha ya ukarimu na vivutio
vya wanyamapori vilivyopo katika ukanda wa Afrika Mashariki, uwepo wa
wanyamapori ndani na nje ya viwanja vya ndege unaleta hatari kubwa na
changamoto kwenye safari za anga.
Idadi ya viwanja
vya ndege katika ukanda wa Afrika Mashariki zinakumbwa na hatari kubwa
ya wanyamapori, kwa sehemu kwa sababu vinajikuta viko karibu na vyanzo
vikubwa vya maji kama bahari,ziwa n.k au viko kwenye njia za kimataifa
zinazotumiwa na makundi ya ndege kuhama sehemu moja kwenda nyingine.
AviAssist husaidia viwanja vya ndege na mashirika ya ndege kuchukua
hatua za awali katika kusimamia hatari ya wanyamapori katika viwanja vya
ndega na maeneo ya karibu na viwanja vya ndege. Shirika linafanya bidii
ili kuhakikisha usalama bora unakuwepo kwa wataalamu wa anga katika
ukanda au karibu na nyumba zao.
Mashirika yote ya ndege ni lazima kuchukua hatua za kupunguza hatari, na
ili kuhakikisha shughuli za viwango vya juu vya usalama, Fastjet
inaendelea kushirikiana na wadau wa usalama wa anga, ikiwa ni pamoja na
shirika la AviAssit, kukuza usimamizi wa usalama katika shughuli zetu”
alisema Kibati.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi wa AviaAsisst Tom Kok alisema kuwa, yeye ana matumaini
kwamba shirika lake litawapatia Fastjet na washirika wake mafunzo bora
zaidi na huduma bora ambazo wateja wanatarajia na wanastahili.
Tumefanya
jitihada kupata mkataba huu, na mteja huyu mpya na tunajisikia fahari
kwamba Fastjet imeichagua AviAssist kama mtoa mafunzo haya muhimu,”
alisema Kok.
Kok Aliongeza
kuwa, mkataba huu kutoka kwa moja ya mashirika ya ndege mapya na yenye
mhemko zaidi barani Afrika, inasisitiza kuongezeka kwa heshima ya soko
ambalo AviAssist inalijenga katika bara la Afrika kwa ubora, gharama
fanisi na utoaji wa wakati wa huduma za kuboresha usalama ambapo kwa
sasa hakuna biashara mbadala ambayo ni yakinifu,”alisema.
Alielezea
kwa kina kwamba, shirika lake linatarajia kujenga biashara zaidi kwa
ajili ya shirika, biashara ambayo kwa upande wake inasaidia moja kwa
moja bidhaa za AviAssist kama vile magazeti yetu ya bure yanayohusu
usalama na makundi ya Facebook ya bure kwa wataalamu wa anga wa Afrika.


No comments:
Post a Comment