Habari toka TAMUNET- Mtandano wa Wanamuziki Tanzania.
KUNDI la Double M chini ya Muumin
Mwinyjuma, limealikwa Msumbiji kwa mwezi mzima, na katika wakati huo
kundi litashiriki katika sherehe za miaka 51 ya Vita vya Ukombozi wa
nchi hiyo.
Wanamuziki hawa ambao ni wanachama wa Mtandao wa Wanamuziki
walipitisha barua yao ya taarifa ya kwenda huko na hivyo Mtandao ukatoa
taarifa Baraza la sanaa La Taifa kama inavyostahili.
Waliomo katika
msafara huo ni pamoja na kiongozi wa kundi Muumin Mwinyjuma, maarufu
kwa jina la KOCHA, na wanamuziki wengine 16. |
No comments:
Post a Comment