![]() |
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
…………………….
TIMU ya soka ya kiluvya United
‘Wabishi wa Pwani’jana walianza vema kivumbi cha ligi daraja la kwanza
baada ya kuichapa timi ya Ashanti united ya Jijini Dar es salaama kwa
mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa mabatibi mlandizi.
Mchezo huo wa ligi daraja la
kwanza ulikuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote mbili kucheza
mpira wa kasi katika dakika za kipindi cha kwanz akwa lengo la kuweza
kuondoka na ushindi na kujinyakulia pointi tatu muhimu lakini hadi hadi
mapumziko hakuna mbambe aliweza kuzifumania nyavu za mwenzake.
Kipindi cha pili timu yakiluvua
united ilionekana kuingia kwa kubadilisha mfumo wa mashambulizi na
kuanza kulisakama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuandika bao la
kwanza kunako katika dakika ya 47 lililowekwa kimiani na mshsambuliji
wao wa kutumaniniwa Chala Juma.
Kuingia kwa bao hilo kuliweza
kulionekana kuwachanganya wachezaji wa Ashanti united kwa kujipanga upya
na kujaribu kuongeza kasi zaidi kwa lengo la kupata bao la kusawazisha
lakini kutokana na safu ya ulizni ya kiluvya united kuwa imara waliweza
kuthibiti mashambulizi ya wapinzani wao.
Mchezaji Kulwa Muanda pamoja na
kimo chake kuwa ni kifupi aliweza kuonyesha uwezo wake katika kulisakata
kabumbu baada ya kuwainua mashambiki wa kiluvva united baada ya
kupachika bao la pili baada ya kuiunganisha krosi safi iliyochongwa
Chala Juma na kuwamwacha mlinda mlango wa Ashanti united amebaki mdomo
wazi.
Ashanti united licha ya kuwahi
kuonja joto la kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara walijikuta wanakabwa
koo na wabishi hao wa Pwani na kupelekea hadi kipenga cha dakika tisini
kinapulizwa timu ya Kilivya ilitoka uwanjani hapo kifua mbele kwa
ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzania wao.
Mara baada ya kumalizika kwa
matanange huo mlezi wa timu hiyo Edward Mgogo almaarufu (Eddo Master)
alisema kwamba vijana wake wameonyesha mchezo mzuri na kupatikana na
ushindi huo ni kutokana na kujituma katika dakika zote za mchezo huo.
Aidha Eddo alisema kwamba ana
imani vijana wake wataweza kufika mbali na kufanya vizuri katika ligi
daraja la kwanza na kuwaomba wadau wa Mkoa wa Pwani mchezo wa kandanda
kwa ujumla sambamaba na wana kiluvya wote kuhakikisha wanaipa
ushirikiano wa dhati timu hiyo katika ligi hiyo ya daraja la kwanza
amabyo inaushindani mkubwa kutokana na kuzishirikisha timu amabzo
zilishawahi kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara.



No comments:
Post a Comment