KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 22, 2015

WADAU WANAOTAKA KUANDAA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA WANATAKIWA

New Picture1 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Kamati ya Miss Tanzania inapenda kuwatangazia wadau wote wanaotaka kuandaa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 kutuma maombi yao ya uwakala kuanzia sasa hadi tarehe 30 Novemba 2015 ndio mwisho wa kupokea maombi ha yo.

Mashindano yatakayo fanyika ni ya mikoa tu, hakutakuwa na mashindano katika ngazi ya kitongoji, wilaya wala Kanda.

Sifa za kuwa Wakala wa Miss Tanzania ni pamoja na

1) Uwe na Kampuni iliyosajiliwa na Mamlaka husika ya Serikali.

2) Uwe na mtaji wa kutosha.


3) Uwe na uwezo wa kuandaa shindano katika ufanisi mkubwa.
 
4) Uwe mstari wa mbele katika kukuza sanaa za utamaduni nchini.

Wakala atakaye pitishwa na Kamati ya Miss Tanzania atapaswa kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa.(BASATA) kabla hajapewa kibali cha kuandaa shindano.

Wilaya za Mkoa wa D’salaam, Ilala, Kinodoni na Temeke zitapewa hadhi ya Kimkoa, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Elimu ya Juu.
  
Ada ya Uwakala ni shilingi milioni moja(1,000,000/-).

Ada ya Uwakala italipwa kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya maombi kukubaliwa na kupitishwa.

Maombi yatumwe kwa barue pepe misstanzania2015@yahoo.com
Kwa mawasiliano na ufafanuzi zaidi piga namba zifuatazo:-

0673 521037 Katibu wa Kamati 0754 337043 Msemaji wa Kamati 0755 019288 Sekretariet.

Imetolewa na:
JUMA PINTO. MWENYEKITI KAMATI YA MISS TANZANIA.

2 comments:

  1. Hi tazama link hii kwa kupata
    muuonekano fresh na fedha juu
    link http://4ui.us/ingiahapa

    ReplyDelete
  2. Hi tazama link hii kwa kupata
    muuonekano fresh na fedha juu
    link http://4ui.us/ingiahapa

    ReplyDelete