Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) akiwa na Mkuu wa Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam Profesa Mohamed Janabi
alipomtembelea leo,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es
salaam,Muadhama, Kardinali Pengo.Picha kwa Hisani ya Wizara hiyo.

WAZIRI wa Afya , Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu , akiongozana na Mkurugenzi
wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi
wakati alipowasili Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, leo ili
kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es
salaam,Muadhama, Kardinali Policarp Pengo . Kulia ni Katibu Mkuu wa
wizara hiyo, Dk Mpoki Ulisubisya


WAZIRI wa Afya , Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu , akimjulia hali mmoja wa
wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo, katika taasisi ya Tiba ya Moyo
ya Jakaya Kikwete,Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, leo.
Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulisubisya na katikati
ni Dakatari bingwa wa upasuaji wa wa moyo kwa watoto Dk. Godwin
Godfrey.
…………………………………………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo-MAELEZO
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la
Katoliki la Dar es salaam,Muadhama, Kardinali Pengo amesema kwamba
ameridhishwa na huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili(MNH), hivyo itakuwa ni vigumu kwa Serikali kumshawishi kwenda
kutibiwa nje ya nchi.
Kauli leo na Askofu Pengo
ambaye amelezwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika
hospitali ya MNH jiji Dar es Salaam kuanzia Januari Mosi, mwaka
2016 hadi sasa mara baada ya kuzungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alimtembelea
leo mchana ili kuweza kufahamu maendeleo ya afya yake.
“Ninapenda kutoa taarifa kwa
umma wa Watanzania na kuwaondoa hofu kuwa hali ya Baba Askofu Pengo
imeimarika na anaendelea vizuri, hajawekewa oxygen wala hajalazwa
katika wodi ya uangalizi maalum(ICU) na ameridhika na huduma
zinazotolewa.
“Ameridhika na huduma
zinazotolewa za moyo, itakuwa ni vigumu sisi kama Serikali kumshawishi
kwenda kutibiwa nje ya nchi, ” alisema Waziri huyo.
Aidha Waziri Ummy alitembelea
sehemu ya ICU, katika taasisi hiyo, ambapo alisema operesheni ambazo ni
ngumu zinafanyika, katika opresheni za moyo kiwango cha kimataifa ni
asilimia 6, wakati Tanzania imefikia kiwango cha asilimia 4, hivyo
tunafanya vizuri.
Aliongeza kwamba hatua hiyo
inapunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi, pia
aliwataka hata wagonjwa kutoka taasisi binafsi kwenda kutibiwa katika
taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa taasisi
hiyo, Profesa Mohamed Janabi alisema Baba Askofu huyo ameridhika na
matibabu aliyoyapata ambayo yanaweza kufanyika Tanzania, hivyo
changamoto iliyopo kwa Serikali kupitia wizara hiyo ni kuiwezesha
taasisi hiyo kibajeti ili kuwezesha wagonjwa anagalau 50 kati ya 300
ambao wako kwenye orodha ya kupatiwa huduma.
Aliongeza kwamba Baba Askofu huyo, ataruhusiwa siku za karibuni, baada ya hali kuendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment