Waziri wa Fedha Mhe,Omar Yussuf
Mzee amesema kuanzishwa kwa Jumuiya ya vijana wa paunia wa zamani (Young
Peoneer Veterani Association ) kutasaidia vijana kujikwamua na
umasikini pamoja na kujiepusha na madawa ya kulevya .
Alisema tunashuhudia vijana wengi
wa Zanzibar wanaendelea kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo madawa
ya kulevya na kupelekea mmong’onyoko wa maadili .
Hayo aliyasema leo huko katika
ukumbi wa ZSSF Kariakoo wakati alipokuwa akizindua Jumuiya mpya
isiyokuwa ya kiserikali Young Peoneer Vererani Association yenye
lengo la kuwasaidia vijana wa Zanzibar kimaendeleo.
Waziri Mzee amekemea tabia ya
vijana kutokuwa na maadili na kujiingiza katika vikundi viovu jambo
ambalo linapelekea kuhatarisha maisha na kwenda kinyume na silka na
utamaduni wa Zanzibar .
“ Hii inaonesha utofauti mkubwa
uliopo wa malezi heshima na tamaduni zilizokuwepo awali zimetoweka
kwa kuvaa nguo zisizostahiki na kupenda maisha ya anasa wakati uwezo wao
ni mdogo.”Alisema Waziri Omari.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa
Jumuiya hiyo kuwa na ushirikiano wa pamoja ili wawe na uwadilivu katika
kazi zao waepukane na tamaa.
Sambamba na hayo Waziri Omari
alianzisha harambee ya papo kwa papo na kuweza kukusanya fedha ya zaidi
ya Tshs millioni 3,834,500 za papo kwa papo na Tshs Millioni 5,850,000
za ahadi jumla shilling millioni 9,724,500 zilichangiwa Jumuiya hiyo .
Hata hivyo Waziri huyo aliahidi
kutoa Komputa mpya moja na Printa mpya moja na pesa taslimu Tshs milioni
moja na laki tano pamoja na Tshs milioni moja kwa ajili ya mchango wa
mkewe ili kuweza kuisaidia jumuiya hiyo .
Nae Katibu wa Uwezeshaji,Ustawi
wa Jamii Vijana,Wanawake na Watoto Asha Ali Abdalla kwa niaba ya Waziri
Uwezeshaji ,Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zainabu Omar
Muhammed alisema ushirikiano wa jumuiya utaleta mafanikio kwa vijana wa
Zanzibar na Jumuiya wasisiste kuitumia wizara yake kwa matatizo mbali
mbali ambayo yatayojitokeza.
No comments:
Post a Comment