
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya
Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amejiuzulu
nafasi hiyo kuanzia leo baada ya kuomba kwa uongozi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini (TFF).
Kaijage aliiongoza Twiga Stars
kwenye fainali za michezo ya Afrika (All Africa Games) zilizofanyika
nchini Congo Brazzavile Septemba mwaka jana, baada ya kuiondoa timu ya
taifa ya Zambia katika hatua ya mtoano.
TFF imesikitishwa na taarifa za
kujiuzulu kwa kocha huyo mwenye leseini A ya CAF, ambaye amekuwa
akizinoa timu za taifa za wanawake ya wakubwa (Twiga Stars) pamoja na
timu ya wanawake wenye umri chini ya miaka ya 20 (Tanzanite) tangu mwaka
2013.
Kufuatia kujiuzulu kwa kocha
Kaijage, TFF inaendelea na programu za maendeleo ya soka kwa wanawake,
ikiwemo kuendesha ligi ya wanawake (Tanzania Women League).
TFF inamtakia kila la kheri kocha Rogasian Kiajage katika shughuli zake.
Aidha maandalizi ya mchezo kati
ya Twiga Stars dhidi ya Zimbambwe yataendelea chini ya kocha
atakayeteuliwa kuchukua nafasi yake, mchezo utakaochezwa mwezi Machi
mwaka huu na mshindi kucheza na Zambia.
TFF itaendelea kupambania kwenye maendeleo ya soka la wanawake.
No comments:
Post a Comment