KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 18, 2016

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII AFRIKA MASHARIKI NA KATI

w3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Vyombo mbalimbali vya Habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa nane wa Mifuko ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika jijini Dar es Salaam.
re
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF  Rehani Athumani akifuatilia mkutano wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya  Jamii Afrika Mashariki uliofanyika leo Jijini Dare s salaam.

re2
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano wa vyama vya mifuko ya Jamii Afrika Mashariki na kati wakiwa wamesimama kumuaga mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam.

re3
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mawaziri na manaibu waziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika ya Mashariki na Kati wakati wa mkutano wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya  Jamii Afrika Mashariki na kati leo Jijini Dar es Salaam.

w1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi cheti katika Mkutano wa Nane wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Makamu wa Rais amefungua rasmi mkutano huo leo katika Ukumbi wa Benki Kuu.

No comments:

Post a Comment