Mtangazaji
wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati),
ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa
chaneli na vipindi vya michezo, akichezesha droo ya kwanza ya bahati
nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi
ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika
ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo
pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif
(kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw.
Abdalla Hemedy (Kulia).
Mkaguzi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy
(Kulia) akiandika namba ya mshindi wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya
kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya
Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika
ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo
pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif
(kushoto) na Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih
Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania
kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo.
Makamu
wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akipiga namba
ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya kwanza ya bahati nasibu
ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya
Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika
ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo
pamoja naye ni Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw.
Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes
Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo na Mkaguzi kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
Mtangazaji
wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati),
ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa
chaneli na vipindi vya michezo akizungumza na mshindi kwa njia ya simu
aliyepatikana wakati wa uchezeshwaji wa droo ya kwanza ya bahati nasibu
ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya
Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika
ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo
pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif
(kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw.
Abdalla Hemedy (Kulia).
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Chuo cha Ualimu cha Mkwawa cha mkoani Iringa ambacho ni chuo
kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bernadeta Killian
(50) amefanikiwa kuibuka mteja wa kwanza mwenye bahati kwa kujinyakulia
tiketi ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga kutoka kwa
kampuni ya StarTimes katika droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Akizungumza
kwa njia ya simu Profesa Killian baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi
amesema kuwa anayo furaha isiyoelezeka kupata taarifa hiyo ya ushindi
ambao hakufikiria kama kuna ofa hiyo nzuri kwa wateja.
“Ninajisikia
furaha kwa kutangazwa kuwa mshindi kwani sikutarajia kama wateja wa
StarTimes tunaweza kupewa kubwa kiasi hiki ya kwenda Ujerumani kutazama
mechi ‘Live’. Naweza kusema mwaka umeanza vizuri kwa kuonyesha dalili ya
neema kama hii, ni fursa kubwa kwangu mimi kama mteja kwani kuna
maelefu ya wateja ambao wangependa kupata fursa hii.
Nawashukuru
kwa hili kwani wameliendesha zoezi bila ya upendeleo na sisi wateja wao
tunafurahi na kuwapongeza sana na tutandelea kuwaunga mkono.” Alieleza
Profesa Killian
Mshindi
huyo wa kwanza wa droo iliyopewa jina la ‘Pasua Anga na StarTimes’
alipatikana baada ya kujiunga na kifurushi cha Super ambacho ni shilingi
36,000/- katika dishi. Lakini pia mteja yoyote wa StarTimes anaweza
kuibuka mshindi kwa kujiunga na kifurushi chochote kuanzia cha shilingi
5,000/- na kuendelea kwa upande wa ving’amuzi vya dishi na antenna. Na
kwa wateja wapya pindi wajiungapo na huduma za kampuni hiyo wamekuwa
wameunganishwa moja kwa moja na droo ya bahati nasibu.
“Ningependa
kutoa wito kwa wateja wenzangu waendelee kujiunga kwani bado nafasi
zimebaki kushindaniwa na zote zipo kwa ajili yao, hivyo wasilaze damu.
Ninaahidi kuitumia fursa hii ipasavyo kwa kuenda kutazama wenzetu wa
ulaya wanafanya nini kwa upande wa soka kwani kwa muda mrefu tumekuwa
tukitazama kupitia kwenye luninga, pongezi tena kwa StarTimes kwa
kuifanya ligi ya Bundesliga ionekane kupitia ving’amuzi vyake kwa
gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Wamefanikiwa kwa
kiasi kikubwa kuipa ligi hiyo umaarufu nchini kwani sasa kwa kiasi
kikubwa michezo yote inaonekana ‘Live’ na kufuatiliwa na watu wengi.”
alihitimisha Mkuu huyo wa Chuo cha Ualimu Mkwawa
Naye
kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi.
Zuhura Hanif amebainisha kuwa, “Hii si mara ya kwanza sisi kuchezesha
droo ya bahati nasibu kwa kuwazawadia wateja wetu ni zawadi mbalimbali,
hivyo basi huu ni muendelezo tu wa ofa nyingi zinazoendelea kumiminwa
kwa wateja wetu waaminifu. Safari hii wateja wetu tumeamua kuwazawadia
safari itakayolipiwa gharama zote na kampuni kwenda Ujerumani kutazama
ligi ya Bundesliga ambayo kwa Afrika ndio kampuni pekee yenye hakimiliki
ya kuionyesha ‘Live’.”
“Makubaliano
baina ya wamiliki wa ligi hiyo ya Ujerumani na kampuni ya StarTimes
yaliingiwa kwa dhumuni kubwa la kuifanya ligi hiyo maarufu barani Afrika
kama ligi zingine. Na ni kwa kupitia StarTimes pekee hilo linaweza
kufanikiwa kutokana na wingi wa wateja wetu, ubora wa huduma na gharama
nafuu ambazo mwananchi yoyote wa kipato cha chini anaweza kuzimudu,”
alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo basi nampongeza mshindi wa leo na
nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga nasi au walipie vifurushi vyao
ili waingie kwenye droo ya bahati nasibu na kujishindia safari hii kubwa
kwenda Ulaya kutazama mechi moja kwa moja pamoja na mashabiki wengine
ulimwenguni.”
Akielezea
machache kutokana na ushuhuda wake baada ya kupata fursa ya kutembelea
ofisi za Bundesliga na kushuhudia mechi kadhaa nchini Ujerumani,
Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda,
ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa
chaneli za michezo, amesema kuwa, “Bahati ya kupata safari ya kwenda
Ujerumani ni fursa kubwa sana kwa wateja na ningependa waitumie vema.
Kuna mengi tu ya kujifunza licha ya kufurahia safari hiyo. Wenzetu
wamepiga hatua kubwa na tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao, hivyo
nawasihi waitumie vemam ili waje kutuhadithia na sie huku.”
Zoezi
zima la uchezeshwaji wa droo ya bahati nasibu ya kumpata mshindi
ilichezeshwa kwa uwazi na haki mbele ya waandishi wa habari ikishuhudiwa
na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
No comments:
Post a Comment