![]() |
Ofisa Mtendaji Mkuu wa UTT-PID Dkt. Gration Kamugisha |
Katika kuhakikisha kwamba taifa linapiga hatua
kubwa ya kimaendeleo na wanachi wanapata huduma bora na kwa wakati Serikali
imeanzisha taasisi mbalimbali za umma mojawapo ya taasisi hizo ni UTT-PID.
UTT –PID, Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya
Miundombinu (UTT-Projects and Infrastructure Development ) ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya
Wizara ya Fedha ambayo ilianza shughuli
zake rasmi Julai Mwaka 2013 .
Ofisa Mtendaji Mkuu wa UTT-PID
Dkt. Gration Kamugisha anasema kuwa taasisi hiyo inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa asilimia mia moja.
Anazitaja kazi kuu za UTT-PID kuwa ni utoaji wa huduma
za ushauri katika maeneo ya Upembuzi
yakinifu wa miradi mbalimbali,maandalizi ya hadidu za rejea’,mipango ya huduma
za kifedha , kuwasilisha miradi na huduma zinazohusiana.
Msingi
wa kuanzishwa kwa taasisi hii na Serikali ni kuweka manzingira wezeshi ili
kupata au kuvutia mtaji binafsi (private capital) katika kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo
sharti iwe inakidhi vigezo vya kuwa na faida za kijamii, kiuchumi na kifedha.
Miradi mingi iliyotekelezwa hadi sasa inahusiana
na uendelezaji wa ardhi na majengo lakini
lengo na mtazamo wa taasisi ni zaidi ya hapo. Ipo miradi mingi na mikubwa
ya kimiundombinu katika sekta za afya, elimu, nishati, nk ambayo imeletwa
kwenye taasisi na wadau mbalimbali hasa taasisi za umma ambayo inatafutiwa
fedha
Dkt. Kamugisha anafafanua kuwa ili taasisi yoyote
ile ipige hatua ni lazima iwe na Dira hivyo kwa upande wao Dira yao ni kuwa
mdau wa maendeleo wa kuaminika katika
fani ya Usimamizi wa Miradi na Maendeleo ya Miundombinu na kuwa na mtazamo wa
uwajibikaji wa dhati ili kutosheleza mahitaji kwa wateja na kuendelea kuboresha
huduma.
“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunawajibika kwa
wateja watu.. na katika hili ni lazima tutoe huduma bora mbazo zinakata kiu ya
wateja wetu” anasema.
Itaendelea Jumatatu....
No comments:
Post a Comment