![]() |
| Ofisa Mtendaji Mkuu wa UTT-PID,Dkt.Gration Kamugisha |
Ijumaa iliyopita tuliangazia historia ya UTT-PID, leo Ofisa Mtendaji Mkuu Dkt.
Gration Kamugisha anaelezea zaidi majukumu mbalimbali ya taasisi yake ...ungana naye.
Anabainisha kwamba Dhamira yao ni kufungua mitaji
iliyodumaa kwa kuwasaidia wateja kitaalam katika maeneo ya miradi na maendeleo ya miundombinu na kuleta ukuaji wa mapato kwa ajili ya
wateja na wadau ambao ni pamoja mwanahisa (serikali). .
“Na katika kutekeleza hilo kuchochea ukuaji wa
uchumi na huduma za kijamii katika sehemu husika ambayo sisi tunahusisha mitaji
iliyo lala,” anasema.
Anasema kwamba mfano wanapokwenda kupanga mji katika
eneo lolote katika nchi yetu, ni wazi kamba barabara zitachongwa, huduma za
umeme zitafika, huduma za maji zitakuwepo, na shughuli nyingine za kiuchumi
zinazoendana na huduma hizo zitafanyika,”
“Kwa hiyo utaona ni dhahiri kwamba wananchi
watafaidika na huduma zinzotokana na uwezekezaji wetu katika eneo husika na
hivyo kuchangia ukiuaji wa uchumi,” anasema.
Lakini pia Dkt. Kamugisha anasema katika
kufanikisha yote hayo ni lazima kuwe na maadili , hivyo suala la maadili kwao
ni kipaumbele pia .
“Tunaongozwa na misingi ya uwajibikaji, uwezo
na motisha kwa wafanyakazi , uhakika
wa ongezeko la wafanyakazi wenye sifa
,kuthamini uvumbuzi ,utambuzi na
maboresho ili kuepuka au kupunguza uwezekano wa kujitokeza kwa
malalamiko”.
Pia katika kuteleleza majukumu yao anasema suala
la ubora wa huduma ni kipaumbele
“Kutekeleza dhana nzima ya utoaji bidhaa /huduma
zenye sifa na thamani ya kipekee huku wakihakikisha kwamba gharama nafuu kwa kujitahidi katika kuboresha
huduma na bidhaa zao” anasema.
Anabainisha kuwa wamekuwa wakijitahidi kutoa
huduma bora kwa wateja wao katika kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kulingana
na thamani ya fedha na hivyo kumridhisha mteja.
“Tunajitahidi sana kukidhi mahitaji ya mteja, kuhakikisha kwamba taasisi inatoa huduma zilizo
bora kwa wateja wao kwa kiwango
kinachokidhi na hata kuzidi matarajio yao,”.
Kuhusu suala la faida
anasema kwamba taasisi yake imejikimu kimsingi katika uwezo wa kuongeza faida
kutokana na uwekezaji wake kama vile....Itaendelea kesho



No comments:
Post a Comment